Thursday 17 April 2014

WAZIRI WASSIRA KATIKA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO


PIX_2_2a7f0.png
Ofisa wa Jeshi la Polisi, Christina Mponji akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (wa pili kushoto) picha za Wakuu wa Jeshi la Polisi mbalimbali toka tulipopata uhuru hadi wa hivi sasa.  Waziri Wassira alilitembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambalo lina Taasisi tatu za Muungano ambazo ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). Maonesho hayo ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanafanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wassira (kushoto) akipokea vipeperushi vya Idara ya Uhamiaji alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Taasisi zake za Muungano katika  Maonesho ya siku tano ya Miaka 50 ya Muungano yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)PIX_3_43102.png

0 comments: