Thursday 17 April 2014

ATLETICO MINEIRO YATISHIA KUMPELEKA MAHAKAMANI ANELKA KWA KUGOMA KWENDA BRAZIL

264816-nicolas-anelka-1 Atletico Mineiro wamejibu shutuma kwamba Nicolas Anelka hakuwa anajua chochote kuhusu suala la uhamisho wa kujiunga na klabu hiyo ya Brazil na hata kufikia hatua ya kutishia kumfungulia mashtaka ya kumdai fidia mchezaji huyo.
Anelka, 35, aliposti video kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook jana Jumatano asubuhi ambapo alionekana kukataa kwamba alikuwa amesaini kujiunga na mabingwa Copa Libertadores .
Hata hivyo,  raisi wa Atletico Mineiro, Alexandre Kalil, amepingana na Anelka, ambaye alimtangaza kumsaini tarehe 6 mwezi huu.
“Tutaelelezea kila kitu kuhusu uhamisho huu, kwa sababu tuna ushahidi wa kila kitu,” Kali aliwaambia waandishi wa habari.
“Tutakwenda FIFA. Itabidi atulipe fidia kwa kila kitu tulichotumia katika gharama za malazi na usafiri.”
Atletico Mineiro walitangaza wiki iliyopita kwamba wamefuta mpango wa kumsajili Anelka baada ya msjambuliaji huyo kushindwa kwenda kwa wakati Brazil.

0 comments: