Thursday 17 April 2014

LUKUVI AJIBU MAPIGO YA WAPINZANI BUNGENI KUHUSU KAULI YA JESHI KUTAWALA NCHI


 
 
April 17 2014 Wajumbe walio upande wa (UKAWA) kwenye bunge la katiba wakiongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba waligoma na kuamua kutoka nje ya bunge hili hapa Dodoma baada ya Profesa Lipumba kumaliza kuzungumza kwamba hawawezi kuendelea na bunge la matusi na ubaguzi.
Kingine kikubwa alichozungumza Prof. Lipumba ni kusikitishwa na kauli ya Waziri Lukuvi aliyoitoa kanisani weekend iliyopita kwamba jeshi litatawala nchi ambapo April 14 2014 gazeti la Mwananchi lilimnukuu Waziri Lukuvi akisema Kanisani ‘tukipitisha serikali tatu jeshi litatawala nchi’
Kama hutoweza kusikiliza sauti yake hapa chini yafuatayo ni baadhi ya makubwa aliyoyazungumza leo asubuhi

‘Ni kweli kwamba kikao hichi nilipanga nisichangie kwa sababu niliona mechi kali tukishindilia watu watakufa, sikusikia vizuri yaliyotokea jana ila mimi sio mnafiki, nampongeza sana Mh. Mrema kwa hotuba yake juzi, Mrema ndio mpinzani wa kweli, alisema angalia mambo yanayotokea Znz msidhani yataishia Magogoni’

‘Baada ya hotuba ya Rais, mh. Seif Sharrif Hamad alihutubia, yeye ni mchochezi wa hovyo kwa kumsingizia Rais, hakuna mtu yeyote anaweza kunizuia kusema ninayoyaamini mimi, sio hapa wala mtaani, ni kweli Jumamosi nilimwakilisha Waziri mkuu ambae hakunipa hotuba na mambo yalinoga nikatawazwa kuwa chifu’

‘Viongozi wa dini waliliombea Bunge pale Kanisani, mimi Waziri nipo pale… nisiongee chochote??!! tukiendeleza ambayo hayako kwenye mila zetu Znz na Tanganyika inaweza kuwa kama Korea kaskazini na kusini, hofu niliyonayo ni juu ya rasimu yenyewe kwa sababu kwanza imejengwa kwenye misingi ambayo siiamini’

‘Zanzibar inatambulika kama nchi kwenye katiba yao toka hata kwenye katiba ya nyuma kabisa, yapo mapungufu muundo wa serikali 3, ukisoma rasimu wanasema serikali ya Tanganyika imevaa koti la muungano lakini koti lenyewe tunapokezana, leo anavaa Mwinyi, leo anavaa huyu’

‘Hatujawahi kutoa bajeti inayotosha kwa jeshi la Wananchi, mmeshawahi ona wanaandamana kudai haki zao? nina miaka zaidi ya 50 na nisingependa kuiona Tanzania hii inakwenda kwenye maisha ambayo sikuyazoea ili kuepusha haya tusijaribu tusichokijua, hii ni hofu yangu… hakuna wa kunizuia kutoa hofu yangu’

‘Ukweli ni kwamba kama umesoma hii rasimu, muundo unaweza kuwa umeandikwa vizuri lakini hauwezi kuwepo, Rais hakutoa vitisho bali mawazo yake kama Mtanzania, hawa jamaa wamekubaliana, serikali ya Znz wachukue CUF, bara CHADEMA na muungano waachiwe CCM’
 Na millard Ayo.COM Dodoma

0 comments: