Saturday 26 April 2014

KUNUSURIKA KUSHUKA DARAJA KWAWAPA SOMO PRISONS!!

1779473_629857920384645_1318975679_nNa Baraka Mpenja wa   Dar es salaam
MAAFANDE wa Tanzania Prisons `Wajelajela` wanasubiri kwa hamu kubwa ripoti ya kocha wao, David Mwamwaja ili waanze kuandaa mikakati mapema kuelekea msimu wa 2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Katika mahojiano maalum na Mtandao huu, Katibu mkuu wa Prisons, Inspekta Sadick Jumbe amesema misimu miwili mfufulizo wamenusurika kushuka daraja, hivyo malengo yao ni kusajili wachezaji wazuri ili msimu ujao washeka nafasi tano za juu.
“Sisi ni viongozi  na tuna majukumu yetu. Tumeona makosa yetu, lakini inapofika mambo ya ufundi, Mwamwaja ndiye mwenye majukumu”.
“Tuna imani na kocha huyo mwenye historia kubwa katika soka. Anaandika ripoti yake ambayo tutaipata ndani ya wiki moja ijayo”.
“Kwa kufuata mapendekezo yake, sisi viongozi tutatekeleza kila alichokiona na kumshauri kwa yetu machache tuliyoyaona kwa nafasi ya viongozi”. Alisema Jumbe.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

0 comments: