Wednesday 30 April 2014

JOSE CHAMELEONE KESHO KUSHEREHEKEA MEI MOSI VILLA PARK MWANZA.

SIKILIZA MPANGO MZIMA.
MSANII Maarufu kutoka nchini Uganda Dr. Jose Chameleone, anaye Sherehekea siku yake ya kuzaliwa leo tarehe APRIL 30, anatarajia kushuka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa burudani ya mtikisiko kwa mikoa ya Mwanza na Geita wakati wa kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi duniani (MEI MOSI na Siku inayofuata).


Meneja wa Burudani wa Klabu ya burudani Villa Park Resort Ramadhan Maganga, alisema kwamba Uongozi wa Villa Park Resort ya jijini Mwanza na Alpha Hoteli ya mkoani Geita wameshirikiana kumleta mwanamziki huyo ili kukata kiu ya wakazi wa mikoa hiyo iliyowashika kwa kipindi kirefu.

“Ni kipindi kirefu watu wanashuhudia kazi zake kupitia Luninga (TV) na kuzisikia kwenye vipindi vya Redio, na chakutamanisha zaidi ni pale wanapoona Chameleone anapozindua nyimbo mpya zilizo kali na kumkosa kwenye majukwaa ya maeneo yao hivyo kuzidisha kiu na hamu, sasa hii ni fursa ya pekee kwao kumshuhudia live akilitawala jukwaa” alisema.

Rama ameongeza kuwa, Dr. Chameleone wa sasa ni tofauti na wa kipindi cha nyuma, kwanza ameongeza orodha ya nyimbo  mpya kali na nzuri zikiambatana na Albam zake zinazokubalika na kupendwa na mashabiki wa burudani ya muziki, pili ameboresha zaidi mitindo ya uingiaji jukwani ikiwemo mavazi yanayo muweka katika hadhi na mwonekano wa juu zaidi kimataifa.

“Ratiba itaanza siku ya MEI MOSI  kwa Dr. Chameleone kutoa show kali kwa wakazi wa Jiji hili (Mwanza) na kutoka sehemu mbalimbali Kanda ya ziwa watakaokuwa mametoka kuhudhulia Maadhimisho ya Sherehe ya Wafanyakazi Duniani kwa kingilio cha shilingi 15,000/= mlangoni watamshuhudia mkali huyo akisindikizwa na Bendi ya Muzuki wa Dansi Super Kamanyola ya jijini hapa” alisema.

Aidha alieleza kuwa kwa sasa Dr. Chameleone aliye maliza ziara yake hivi majuzi nchini Uingereza akitamba na nyimbo zake kali kama Valuvalu, Badilisha na wimbo wake mpya wa Tubonge, ameahidi kutoa Burudani ya kiwango zaidi tofauti na kile kilichozoeleka na mashabiki wake.

Burudani ya Disco na Muziki wa Mwambao iko palepale kama ilivyo kawaida ya siku zote, hivyo watakaolipa kingilio cha sh. 15,000/= mlangoni watapata fursa ya kushuhudia burudani yote bila kutozwa tena kingilio cha ziada mlangoni.

“Ratiba ya burudani kwa mwanamuziki Dr. Chameleone itamalizikia kwa kufanya show kali kwa wakazi wa Mji wa Geita na maeneo ya jirani siku ya Ijumaa, Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa Omega Resort Hotel  kwa kingilio cha shilingi 15,000/= tu mlangoni”alisema

Meneja huyo ametoa wito kwa wapenzi wa burudani na wafanyakazi bora watakaozawadiwa kusherehekea kwa pamoja ndani ya Villa Park Resort pamoja na kupata show kali kutoka kwa Dr. Chameleone ambapo pia kutakuwa na chakula na vyinywaji mbalimbali, ulinzi wa mali umeimalishwa kwa asilimia 100, akiwataka wapenzi wa burudani kuwahi ili kupata nafasi na tiketi zitapatikana mlangoni tu.
HAPPY BIRTHDAY DR. JOSE CHAMELEONE
Say's G. Sengo.

0 comments: