Wednesday 30 April 2014

WAFANYAKAZI 'KATIBA NA SHERIA ' WAASWA KUCHPA KAZI

 ts Baraza 2
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde. (Picha na Martha Komba – Wizara ya Katiba na Sheria).
Baraza 1
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014).
Baraza 3


Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika leo (Alhamisi April 30, 2014) jijini Dar-es-salaam.
“Uwajibikaji ni suala muhimu sana katika utumishi wa umma,” alisema katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar-es-salaam.
Aidha, Katibu Mkuu huyo aliwasihi watumishi wote wa Wizara yake kuungana na wafanyakazi wote nchini na duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi zinazofanyika kesho (Alhamisi, Mei 1, 2014).
Awali akiongea katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.
“Tunapodai maslahi ni lazima pia tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu hizi wafanyakazi wote, wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai maslahi bora,” alisema Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya Wizara hiyo.
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia na kuridhia Taarifa ya Mpango wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2014/2015. 

Na Martha Komba, Dar es Salaam

0 comments: