Tuesday 29 April 2014

FALCAO: SINA WIVU NA MAFANIKIO YA ATLETICO


MSHAMBULIAJI wa klabu ya Monico, Radamel Falcao amesisitiza kuwa haionee wivu klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid kutokana na mafanikio yake msimu huu.
Nyota huyo raia wa Colombia aliondoka Vicente Calderon majira ya kiangazi mwaka jana na sasa kikosi cha Diego Simeone kimepata mafanikio bila yeye kwa kuongoza La Liga na kufanikiwa kufika nusu fainali ya UEFA.
Hata hivyo, mchezaji huyo wa zamani wa Porto amesena anafurahi kuona klabu yake ya zamani inafanya vizuri na anataka kuona inafanikiwa zaidi.
“Sina tatizo lolote na Atletico” . Amezungumza na Mundo Deportivo.
“Najisikia furaha kwa kile kinachotokea katika klabu. Nilijenga urafiki na kuwa na furaha zaidi nilipokuwa pale”.
“Katika maisha ya wachezaji kuna mabadiliko na huwezi kuwa na kila kitu.”
“Ninafuarahia kwa wanachokifanya na nawatakia mafanikio makubwa zaidi”.
Falcao kwa sasa yuko nje ya uwanja  kutokana na majeruhi, lakini anatarajia kushiriki michuano ya kombe la dunia nchini Brazil majira ya kiangazi mwaka huu.

0 comments: