Tuesday 29 April 2014

HIVI NDIVYO CECH, TERRY, ETO`O, HAZARD WANAVYO IPASHIA ATLETICO MADRID KESHO


Inashangaza: Petr Cech akitembea na Nathan Ake (katikati) na Marco van Ginkel kuelekea katika mazoezi.

JOSE Mourinho ameanza maandaliza ya mechi ya kesho ya nusu fainali ya pili ya UEFA dhidi ya Atletico Madrid, huku ikishangaza kumuona mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Petr Cech akifanya mazoezi.

Cech aliteguka beka katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana Vicente Calderon na Mourinho alithibitisha wiki iliyopita kuwa kipa huyo anahitaji upasuaji ili kurudisha bega katika hali yake.
 Nyota wa samba: Willian, David Luiz, Ramires na  Oscar wakielekea katika uwanja wa Coham tayari kwa mazoezi.

Haikuwa rahisi kumouna Cech leo hii ambaye alitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu, hivyo imeshangaza kumuona mchezaji huyo akiwa miongozi kwa wachezaji waliofanya mazoezi leo hii.

Alipoulizwa kama yuko imara kwa mechi ya kesho, alitabasamu na kusema “Ndiyo”, lakini alienda zake na kujiunga na wenzake.

Cech alionekana akifanya mazoezi mepesi leo hii, na makipa wenzake Mark Schwarzer, Henrique Hilario na Mitchell Beeney  walipoanza mazoezi na kocha wa makipa, Christophe Lollichon, Cech  alikaa pembeni.
Mbali na Cech, wachezaji wengine waliokuwa majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao wamefanya mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.

0 comments: