Sunday 27 April 2014

UBALOZI WA TANZANIA NIGERIA WAADHIMISHA MIAKA 50 YA MUUNGANO

 
???????????????????????????????Balozi wa Tanzania chini  Nigeria Mh. Daniel Ole Njoolay akifungua kongamano la Biashara na uwekezaji katika Hoteli ya Serena jijini Abuja Nigeria ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizoandaliwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria. 
???????????????????????????????Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB Bibi Teddy Mapunda akizungumza wakati  Alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii   Tanzania katika kongamano la biashara na uwekeza jijijini Abuja nchini Nigeria. 
???????????????????????????????Mh. Daniel Ole Njoolay, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria akikata keki huku akishuhudiwa na mwakilishi wa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (wa pili kulia) na baadhi mabalozi wanaowakilisha nchi zao Nigeria katika tafrija iliyotayarishwa na ubalozi wa Tanzania.
???????????????????????????????Kikundi cha  ngoma za asili cha Abuja Nigeria  kikitoa burudani ya ngoma katika tafrija kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .
……………………………………………….
Na  Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria
Jumuiya ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria kwa ujumla, wameombwa kuja kuwekeza na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana nchini Tanzania 
Hayo yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi waTanzania nchini Nigeria na kufanyika katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la Biashara na Uwekezaji, Njoolay alisema Tanzania inajivunia muungano wake ulioasisiwa na Hayati Baba waTaifa Mwl Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa Zanzibar mnamo tarehe 26 April, 1964 ambao sasa umetimiza miaka 50.
“Watanzania tunajivunia sana muungano wetu kwani ni wakipekee sana hapa barani Afrika, na ni muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko muungano wowote ule Barani Afrika”…alisema BaloziNjoolay.
Akizungumzia kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa TANTRADE Bwana Edwin Rutageruka alisema kwamba mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizi mbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara kati yake na Nigeria. 
Akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vilivyomo katika orodha ya maajabu 7 ya asili barani Africa, Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB Bibi Teddy Mapunda alisema pamoja na vivutio vitatu (3) vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi yaTaifa ya Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya kipekee na akabainisha kuwa imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutangaza vivutio vyake saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo katika maajabu Saba ya asili barani Afrika, vivutio vingine ni hifadhi ya taifa ya Ruaha, Hifadhi yaTaifa ya Kituro, hifadhi yaTaifa ya Gombe na Pori la akiba la Selous.
Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea Tanzania na kujionea uzuri na upekee wa vivutio vya Tanzania.
Kongamano hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Nigeria mia moja lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku katika hoteli hiyo na kuhuidhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwemo Mabalozi wa mataifa mbalimbali nchini Nigeria, wageni kadhaa mashuhuri na baadhi ya watanzania waishio nchini Nigeria.

ASIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NIGERIA

1-Asia Idarous akiwa na vazi la Kitanzania  
Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye  onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria.2- keki ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania , Abuja Nigeria 
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria. 
3-Fatma Mwinyi 
Fatma Mwinyi akiwa kwenye pozi katika onyesho hilo la miaka 50 ya muungano Abuja Nigeria6-Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania 
Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania
Na Andrew Chale
MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho  kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa  ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota  tano ya Sheraton Abuja, usiku wa  April 25,  huku likiudhuriwa na watu wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na balozi anayewaiwakilisha  Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole
Njoolay.
Akizungumza na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria,  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa kuandaa onyesho hilo maalum,  kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
“Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai kutoka  Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho hilo.  Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda, Fatma Mwinyi, Salma Maulid  na wengine wengi.
 “Utanzania wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha  ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
 Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija  na hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi.

0 comments: