MCHEZAJI
mpya wa Chelsea, Cesc Fabregas amedaiwa kuzinguana na kocha wake wa
timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque hadi kufukuzwa mazoezini
nchini Brazil.
Hasira
zimekuwa za hali ya juu katika kambi ya Hispania baada ya timu hiyo
kuvuliwa ubingwa na kutolewa mapema Kombe la Dunia kwa kufungwa na
Uholanzi na Chile.
Del Bosque hakuvtiwana ufanyaji mazoezi wa Fabregas katakana na kutofuata maelekezo yake.
Nipishe, nenda nje: Hamkani si shwari katika kambi ya Hispania
Baada
ya kuona kuchoshwa na haki hiyo, Del Bosque akamtaka Fabregas ague bipu
na kumkabidhi Xabi Alonso na kuondoka kabisa mazoezini.
Nyota
huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona alichukizwa na jambo hilo, huku
wachezaji wenzake wakimzuia kubishana zaidi na Del Bosque.
Inaaminika
Fabregas alikasirishwa na kutolewa kwa Hispania na pia kuingizwa kama
mchezaji wa tatu wa kutokea benchi katika kipigo cha 5-1 kutoka kwa
Uholanzi, na kutotumika kabisa dhidi ya Chile.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 jumla amecheza dakika 12 tu katika Kombe la Dunia mwaak huu hadi sasa.
Del
Bosque anafahamika kama mtu mwenye huruma sana na mwepesi kusamahe na
haitakuwa ajabu Fabregas akianza katika mchezo wa mwisho wa Hispania
dhidi ya Australia, kocha huyo akijaribu kutafuta kikosi kipya cha
kumtoa mrithi japo kwa ushindi wa mechi moja.
0 comments:
Post a Comment