Amisom:Al Shabaab yapata kipigo Somalia
Wanajeshi wa Kenya walio chini
ya Muungano wa Afrika, wameshambulia kambi za wapiganaji wa al Ahabaab
huku idadi kubwa ya wapiganaji hao wakiuawa.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jeshi la Muungano wa Afrika nchini Somalia.Wanajeshi hao walianzisha operesheni yao mwezi Machi katika juhudi zao za kukomboa miji ambayo bado imetekwa na wapiganaji hao.
Wanajeshi wa Amisom, walifanya mashambulizi ya angani kama sehemu ya operesheni yao kuharibu uwezo wa kijeshi wa Al Shabaab.
Kwa mujibu wa taarifa za wanajeshi hao, ndege za kivita za Kenya ndizo zilizofanya mashambulizi hayo.
Mashambulizi dhidi ya Al Shabaab yanakuja wiki moja baada ya Al-Shabaab kukiri mashambulizi mawili yaliyowaua watu sitini , ingawa serikali ililaumu wanasiasa kwa kuchochea mauaji hayo.
Al Shabaab ilikiri kufanya mashambulizi hayo kama hatua ya kulipiza kisasi kwa wanajeshi wa Kenya kuwepo Kusini mwa Somalia, kama sehemu ya operesheni ya Amisom.
AU imesema kuwa mashambulizi ya angani yaliyofanywa katika eneo la Anole, yaliwaua wapiganaji 30 wa Al shabaab huku wengine 50 wakiuawa katika eneo la Kuday.
Hata hivyo bado ni vigumu kuthibitisha idadi kamili ya wanjeshi waliouawa katika mashambulizi hayo.
0 comments:
Post a Comment