WAKATA miwa wa Mtibwa Sugar wanaendelea kufanya mazungumzo na wachezaji waliopendekezwa na kocha mkuu, Mzalendo, Mecky Mexime ili kurejea katika ushindani.
Afisa habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru
Lugalambwike amesema mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote wataweza
kuwasainisha wachezaji ambao hakuwa tayari kuwataja.
“Kwa miaka miwili hatujafanya vizuri, msimu wa
2012/2013 tulishika nafasi ya tano. Msimu wa 2013/2014 tumeshika nafasi ya
saba. Tunakiri miaka miwili klabu yetu haijafanya vizuri”. Alisema Kifaru.
“Lakini kwetu ni changamoto, tumeweza kubaini
kasoro mbalimbali ambazo tunazifanyia kazi sasa, ikiwa ni pamoja na kunasa saini
za wachezaji wazuri ambao wataifikisha Mtibwa katika ushindani”.
Hata hivyo, Tobias Kifaru alisema inasadikika kuna
baadhi wachezaji wao Salvatory Ntebe, Juma Mpakala, Yusuf Nguya wamejiunga na
Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, lakini hawajui chochote.
Wakati huo huo, Afisa
habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alifafanua kuwa wamewasajili wachezaji hao
watatu kutoka Mtibwa Sugar kwasababu wako huru baada ya kumaliza mikataba yao.
Bwire aliongeza kuwa Ruvu Shooting ni klabu makini
na inafanya kazi kwa mapendekezo ya kocha wao Tom Alex Olaba na ndio maana
waliwasainisha mikataba wachezai hao.
Bado Mtibwa wameendelea kubolewa baada ya beki wao
wa kushoto Paul Ngalema kujiunga na klabu ya soka ya Ndanda fc ya Mtwara, huku
beki wao wa kulia, kinda Hassan Ramadhan Kessi akiwindwa na klabu za jijini Dar
es salaam
Kifaru alisema
kuwa hata mlinda mlango wao bora msimu uliopita, Hussein Sharif `Casillas` yupo
kwenye rada za klabu kubwa, lakini wao hawajatangaza nani wanamuacha na nani
anabaki.
Kifaru akabainisha kuwa kuna wachezaji wamemaliza
mikataba na klabu hiyo, hivyo hawana tatizo nao, lakini kwa wale ambao wana
mikataba, na timu nyingine zinawahitaji, basi wanasubiri mazungumzo.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment