Thursday 26 June 2014

KOMBE LA DUNIA: AGUERO NJE, URGUAY KUMKATIA RUFAA ‘MFUNGWA’ SUAREZ!!


WAKATI Straika wa Argentina Sergio Aguero akiripotiwa kuwa nje ya Kombe la Dunia, Uruguay imeazimia kukata Rufaa FIFA kupinga Adhabu kubwa katika Historia ya Kombe la Dunia alietandikwa nayo Straika wao Luis Suarez.
SOMA ZAIDI:
KIFUNGO MIEZI 4: LUIS SUAREZ KUKATA RUFAA!
SUAREZ-SHANGILIA_URUGUAYUruguay imeamua kukata Rufaa kupinga Adhabu kali alizopewa Straika wao Luis Suarez kufuatia kupatikana na hatia ya kumuuma Mebo Beki wa Italy Giorgio Chiellini.
Rais wa FA ya Uruguay, Wilmer Valdez, amesema: “Adhabu ni kali mno kwa Faulo ile.”
Hii Leo, FIFA ilitangaza kumfungia Miezi Minne Suarez kutoshiriki chochote kwenye Soka baada ya kupatikana hatia na pia amefungiwa Mechi 9 za Kimataifa kuanzia Mechi ya Uruguay ya Jumamosi ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya Kombe la Dunia dhidi ya Colombia zitakazomfanya awe nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Adhabu hii pia inamaanisha atazikosa Mechi 9 za kwanza za Klabu yake Liverpool za Ligi Kuu England kwa Msimu mpya.
Pamoja na Vifungo hivyo, Suarez pia ametandikwa Faini ya Dola 111,000.

SUAREZ-Adhabu zake:
-Kifungo cha Miezi Minne kwa shughuli zote za Soka ikiwa pamoja na kutoruhusiwa kukanyaga Uwanja wowote wa Soka.
-Kifungo Mechi 9 za Kimataifa kuanzia Mechi ya Uruguay ya Jumamosi ya Raundi ya Pili ya Mtoano ya Kombe la Dunia dhidi ya Colombia
-Faini Dola 111,000
**Adhabu hizi inamaanisha atazikosa Mechi 13 za Liverpool, 9 za Ligi na nyingine 4 za Mashindano mengine.

Hata hivyo FIFA imefafanua Suarez hazuiwi kuihama Liverpool ikiwa atataka kama inavyodaiwa kuwa huenda akaenda Spain kuchezea ama Barcelona au Real Madrid.
Tukio hili la kumng’ata Meno Chiellini lilitokea Juzi Jumanne kwenye Mechi ya mwisho ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia ambayo Uruguay iliifunga Italy 1-0 na kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano.SERGIO_AGUERO
Hii ni mara ya 3 kwa Suarez kuadhibiwa kwa kung’ata Meno Wapinzani kwenye Mechi na mara ya kwanza ni Mwaka 2010 huko Uholanzi, Suarez alipofungiwa Mechi 7 kwa kumuuma Kiungo wa PSV Eindhoven Otman Bakkal na mara ya pili ni Aprili 2013, alipofungiwa Mechi 10 kwa kumuuma Meno Beki wa Chelsea BranislavIvanovic kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
AGUERO NJE KOMBE LA DUNIA
Straika wa Argentine Sergio Aguero atakuwa nje ya Kombe la Dunia baada kuumia kwenye Mechi dhidi ya Nigeria waliyoshinda 3-2 hapo Jana Jumatano.
Ingawa Kambi ya Argentina huko Brazil haijathibitisha hili, habari za kuaminika toka Mji Mkuu wa Argentina, Buenos Aires, zimedai Straika huyo amechanika musuli Mguuni.
Kwenye Mechi na Nigeria, Aguero alitolewa baada ya Kipindi cha Kwanza na Kocha Alejandro Sabella alieleza ni sababu ya tatizo la Musuli.
Mechi ijayo ya Argentina ni ile ya Raundi ya Mtoano hapo Julai 1 huko Sao Paulo dhidi ya Switzerland.

0 comments: