NIGERIA
imetanguliza mguu mmoja hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia kufuatia
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bosnia jana mjini Cuiaba katika mchezo wa
Kundi F.
Shukrani
kwake mshambuliaji wa Stoke City, Peter Odemwingie aliyefunga bao hilo
pekee la ushindi dakika ya 29 dhidi ya timu ya mchezaji mwenzake wa
kjlabu hiyo ya England, Asmir Begovic, akimalizia kazi nzuri ya Emmanuel
Emenike.
Timu
hiyo ya Edin Dzeko inaaga Kombe la Dunia baada ya kufungwa mechi mbili
mfulullizo, baada ya awali kufungwa 2-1 na Argentina katika mchezo wa
kwanza, ingawa itacheza mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Iran.
Cheupe dawa; Mshambuliaji Peter Odemwingie akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Nigeria bao muhimu usiku wa kuamkia leo |
Nigeria
sasa inatimiza pointi nne na kukaa nafasi ya pili nyuma ya Argentina
ambayo tayari imefuzu kwa pointi zake sita. Nigeria itaomba sasa Bosnia
ijikaze na kuibana japo kwa sare Iran, ili hata kama Super Eagles
itafanyiwa roho mbaya na Argentina iweze kufuzu 16 Bora.
Iran
ina pointi moja na kama ikiifunga Bosnia itafikisha pointi nne maana
yake kama Nigeria itafungwa na Argentina timu ya pili ya kufuzu kwenda
16 Bora kutoka kundi hilo, itaamuliwa kwa wastani wa mabao ya kufunga na
kufungwa. Kikosi cha Nigeria kilikuwa: Enyeama, Oshaniwa, Yobo, Omeruo,
Ambrose, Onazi, Mikel, Babatunde/Uzoenyi dk75, Musa/Ambeobi dk66,
Odemwingie na Emenike.
Bosnia-Herzegovina:
Begovic, Mundza, Sunjic, Spahic, Lulic 6/Salihovic dk58, Besic,
Misimovic, Medunjanin/Susic dk64, Hajrovic/Ibisevic dk57, Pjanic na
Dzeko.
Mshambuliaji wa Nigeria, Peter Odemwingie (kushoto) akimfunga kipa wa Bosnia Asmir Begovic
0 comments:
Post a Comment