Thursday 26 June 2014

KOMBE LA DUNIA: RONALDO AIPA USHINDI PORTUGAL LAKINI WATOLEWA NJE!



>>GHANA NAO NJE, GERMANY, USA ZASONGA!!
PORTUGAL 2 GHANA 1
RONALDO-AKIRICristiano Ronaldo ameifungia Portugal Bao la ushindi walipoipiga Ghana 2-1 lakini hiyo haikutosha kwani wote wawili walitupwa nje ya Kombe la Dunia na Germany na USA kutinga Raundi ya Pili toka Kundi G.
Portugal walitangulia kupata Bao la kujifunga mwenyewe Beki John Boye lakini Asamoah Gyan aliisawazishia Ghana kwa Kichwa.
Dakika ya 80, Ronaldo alitumia makosa ya Difensi na kuipa Portugal Bao la Pili lakini walishindwa kupata Bao 3 zaidi ambazo zingewafikisha Raundi ya Pili kwani kwenye Mechi nyingine ya Kundi lao Germany iliifunga USA 1-0 ambao wamefungana kwa Pointi na Portugal lakini wana ubora wa tofauti ya Magoli.
Matokeo hayo yaliifanya Portugal iungane na Ghana nje ya Mashindano na Germany na USA kusonga.
VIKOSI:
Portugal: Beto, Joao Pereira, Pepe, Bruno Alves, Veloso, Joao Moutinho, William Carvalho, Ruben Amorim, Nani, Ronaldo, Eder
Akiba: Eduardo, Vieirinha, Ricardo Costa, Luis Neto, Rafa, Meireles, Varela.
Ghana: Dauda, Afful, Boye, Mensah, Asamoah, Atsu, Rabiu, Agyemang-Badu, Andre Ayew, Waris, Gyan
Akiba: Adams, Inkoom, Opare, Essien, Afriyie, Jordan Ayew, Adomah, Sumaila, Wakaso, Kwarasey.

REFA: Nawaf Shukralla (Bahrain).

KUNDI G
TIMU P W D L F A GD PTS
Germany 3 2 2 0 7 2 5 7
United States 3 1 2 0 4 4 0 4
Portugal 3 1 1 1 4 7 -3 4
Ghana 3 0 1 2 4 6 -2 1
USA 0 GERMANY 1
Bao la Dakika ya 55 la Thomas Muller limeipa ushindi Germany kwenye Mechi yao ya mwisho ya Kundi GMULLER_n_KROOSwalipocheza na USA na kutwaa Nambari Wani kwenye Kundi hilo na kutinga Raundi ya Pili ya Mtoano.
Ingawa wamefungwa, USA nao wamesonga Raundi ya Pili kwa ubora wa Magoli kufuatia kufungana kwa Pointi na Portugal ambayo Leo iliifunga Ghana 2-1.
VIKOSI:
USA: Howard; Johnson, Gonzalez, Besler, Beasley; Beckerman, Jones; Zusi, Bradley, Davis; Dempsey
GERMANY: Neuer; Boateng, Mertesacker, Hummels, Höwedes; Lahm (C), Schweinsteiger; Özil, Kroos, Podolski; Müller
REFA: Ravshan Irmatov [Uzbekistan]
KOMBE LA DUNIA
RATIBA/MATOKEO:
MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI
**Saa za Bongo
JUMATATU, JUNI 23, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Australia 0 Spain 3 B Arena da Baixada
1900 Netherlands 2 Chile 0 B Arena Corinthians
2300 Croatia 1 Mexico 3 A Arena Pernambuco
2300 Cameroon 1 Brazil 4 A Nacional
JUMANNE, JUNI 24, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Italy 0 Uruguay 1 D Estadio das Dunas
1900 Costa Rica 0 England 0 D Estadio Mineirão
2300 Japan 1 Colombia 4 C Arena Pantanal
2300 Greece 2 Ivory Coast 1 C Estadio Castelão
JUMATANO, JUNI 25, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 Nigeria 2 Argentina 3 F Estadio Beira-Rio
1900 Bosnia-Herzegovina 3 Iran 1 F Arena Fonte Nova
2300 Honduras 0 Switzerland 3 E Arena Amazonia
2300 Ecuador 0 France 0 E Estadio do Maracanã
ALHAMISI, JUNI 26, 2014
SAA MECHI KUNDI UWANJA
1900 United States 0 Germany 1 G Arena Pernambuco
1900 Portugal 2 Ghana 1 G Nacional
2300 South Korea v Belgium H Arena Corinthians
2300 Algeria v Russia H Arena da Baixada
RAUNDI YA PILI YA MTOANO

JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 49 Brazil v Chile Mineirão Belo Horizonte
2300 50 Colombia v Uruguay Maracanã Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 51 Netherlands v Mexico Castelao Fortaleza
2300 52 Costa Rica v Greece Pernambuco Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 53 France v Nigeria Nacional Brasilia
2300 54 Germany v 2H Beira-Rio Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA MECHI NA MECHI UWANJA MJI
1900 55 Argentina v Switzerland Corinthians Sao Paulo
2300 56 1H v USA Fonte Nova Salvador

0 comments: