Saturday 28 June 2014

DAVID MOYES AULA GALATASARAY, AFIKA NA KUFANYA MAZUNGUMZO...



Target: The former Manchester United boss looked relaxed as he touched down in Istanbul
Anawindwa: Kocha wa zamani wa  Manchester United alionekana mwenye furaha baada ya kugusa ardhi ya  Istanbul.

 

DAVID Moyes amepewa ofa ya mwaka mmoja wenye thamani ya paundi milioni 4 ili arithi mikoba ya  Roberto Mancini katika nafasi ya kocha mkuu wa Galatasaray.
Moyes anarudi kazini mapema baada ya kufukuzwa Manchester United mwezi aprili mwaka huu baada ya kufanya kazi kwa miezi tisa tu katika mkataba wake wa miaka mitano.
Katika utawala wake Man united, Moyes alishindwa kuipa makali baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu kufundisha soka.
Moyes alishawasili mji mkuu wa Uturuki na kufanya mazungumza na leo hii jumamosi nchini kwake Scotland.
Mazungumzo ya pande mbili yamekwenda vizuri na kuwaacha  Waturuki wakiamini kuwa tayari wameshamnasa  mtu wao.
Arrival: David Moyes was in Istanbul but is understood to be cautious about a move toe Turkey
Anawasili: David Moyes alikuwa mjini Istanbul, lakini inafahamika kuwa tayari dili la kujiunga na klabu ya huko limekamilika.
Sunning it up: Since being sacked as Manchester United boss David Moyes has enjoyed a holiday in Miami
Hana shida: Tangu afukuzwe kazi Manchester United, David Moyes amekuwa akila maisha Miami
Poor: Moyes was sacked as Manchester United boss in April with them seventh in the Premier League
Main men: Jurgen Klinsmann (left) and Joachim Low (right) are Galatasaray's top two managerial targets
Jurgen Klinsmann (kushoto) na Joachim Low (kulia) wanawindwa zaidi na Galatasaray.

Galatasaray ndani, Fenerbahce nje

Licha ya kumaliza nafasi ya juu katika ligi kuu ya Uturuki msimu uliopita,  Fenerbahce hawatacheza UEFA wala ligi ya Europa msimu ujao. Mwezi Julai 2012, UEFA iliwafungia kutoshiriki michuano ya Ulaya kwa misimu miwili baada ya kukutwa na hatia ya kupanga matokeo. Wakala wa Uturuki, Muzzi Ozcan aliyeshughulikia suala la Mancini alisafiri kutoka London kwenda Istanbul jana ijumaa kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.
Galatasaray  walithibitisha kuwepo kwa kikao baina ya rais wa klabu, Unal Aysal na Moyes, lakini mazungumzo yalikuwa ni kubadilishana mawazo na walisema  Joachim Low na Jurgen Klinsmann ndio makocha wanaowahitaji.
"Rais ameshatoa hotuba juu ya hilo," alisema msemaji wa Galatasaray.
"Alisema kwamba tumezungumza na David Moyes na alisema kwamba yeye sio chaguo la Galatasaray";
"Walikuwa wanabadilishana mawazo tu. Ni kweli Rais amezungumza na David Moyes".
'Hatuna haraka, tunasubiri kombe la dunia limalizike. Watu wawili tunaowataka ni Low au Klinsmann.'.

0 comments: