Sunday, 22 June 2014

ANGALIA: UJERUMANI KUPIGWA NA GHANA KOMBE LA DUNIA, SARE 2-2


BAO la Miroslav Klose dakika ya 71 limeinusuru Ujerumani kulala mbele ya Ghana, baada ya kulazimisha sare ya 2-2 usiku huu katika mchezo wa Kundi G Kombe la Dunia mjini Fortaleza, Brazil. Klose sasa amefikisha jumla ya mabao 15 katika Kombe la Dunia na kumfikia mfungaji bora wa kihistoria wa michuano hiyo, Mbrazil Ronaldo Lima, ambaye tayari ametungika daluga.
Asamoah Gyan akishangilia na wenzake baada ya kuifungia Ghana bao la pili lililokaribia kuwa la ushindi
Miroslav Klose akiondoka kushangilia baada ya kuisawazishia Ujerumani dhidi ya Ghana usiku huu
Mario Gotze alianza kuifungia Ujerumani dakika ya 51, lakini Andre Ayew akaisawazishia Ghana dakika ya 54 kabla ya Asamoah Gyan kuifungia Black Stars bao la pili dakika ya 63. Ghana wakashindwa kuulinda ushindi wao na Klose akaisawazishia Ujerumani dakika ya 71. Beki wa Arsenal, Per Mertesacker ametimzia mechi 100 za kuichezea Ujerumani ikibaki kileleni mwa kundi hilo kwa kutimiza pointi nne kutokana na ushindi wa 4-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Ureno, wakati Ghana inaokota pointi ya kwanza leo baada ya awali kulala 2-1 kwa Marekani. Kikosi cha Ujerumani kilikuwa; Neuer, Howedes, Hummels, Khedira/Schweinsteiger dk69, Ozil, Muller, Lahm, Mertesacker, Kroos, Gotze/Klose dk69 na Boateng/Mustafi dk46. Ghana; Dauda, Gyan, Atsu/Wakaso dk72, Boateng/J Ayew dk53, A Ayew, Muntari, Rabiu/Badu dk78, Mensah, Asamoah, Boye na Afful.

0 comments: