Tuesday 24 June 2014

YAYA TOURE AZIDI KUISAKAMA KLABU YAKE MAN CITY!!

>>ALAUMU KUNYIMWA RUKSA AWE NA NDUGU YAKE ALIEFARIKI WAKATI AKIWA MAHUTUTI!
YAYA_TOURE-GOLI_100YAYA TOURE amezidi kukoroga hali yake ya baadae na Klabu yake Manchester City baada ya kushusha tuhuma nzito kwamba walimnyima ruksa ili awe na Ndugu yake aliekuwa akiugua na hatimae kufariki.
Mdogo wake Yaya Toure, Ibrahim, alikuwa akiugua saratani na hatimae kufariki Wiki iliyopita.
Yaya Toure, pamoja na Ndugu yake Kolo Toure, hivi sasa wako Brazil na Timu ya Ivory Coast wakishiriki Fainali za Kombe la Dunia.
Akiandika Makala kwenye Jarida la France Football, Toure alidai mara baada ya kumalizika Msimu wa Ligi huko England, ambapo yeye alitoa mchango mkubwa kuipa Ubingwa Man City, yeye aliomba ruksa ili amuuguze Nduguye kabla hajajiunga na Ivory Coast kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia lakini alikataliwa.
Badala yake alilazimika kusafiri na Man City kwenda Abu Dhabi, Nyumbani kwa Wamiliki wa Klabu, ili kusheherekea kuchukua Ubingwa wa England.

Toure ameeleza: “Naungama najisikia mwenye huzuni mno. Bado naumia kwa sababu sikumsaidia lolote Siku zake za mwisho. Nilitaka kuwa nae badala yake nikaenda Abu Dhabi. Najilaumu mwenyewe kwa kutolazimisha.”
Tangu Msimu wa England umalizike, hii ni mara ya pili kwa Yaya Toure kuisakama Klabu yake na mara ya kwanza alilalamika kutoheshimiwa baada ya Klabu hiyo kusahau na kutoithamini Siku yake ya Kuzaliwa.

Wachambuzi wanahisi ama Toure anataka kulazimisha kuhama au analeta kashikashi ili aboreshewe Mkataba.

0 comments: