>>KUNDI(B): NANI KUMALIZA KILELENI ‘KUMKWEPA MWENYEJI’ BRAZIL?
JUMATATU
Usiku Makundi A na B ya Fainali za Kombe la Dunia yatacheza Mechi zake
za mwisho na wakati Kundi B tayari Netherlands na Chile zimefuzu kuingia
Raundi ya Pili ya Mtoano ya Timu 16, Kundi A bado zipo Timu 3
zinazogombea nafasi mbili.
Kwenye Kundi A, Wenyeji Brazil, Mexico
na Croatia ndizo zinazowania nafasi mbili za kucheza Raundi ya Pili huku
Cameroon ikiwa nje ya Mashindano.
Kundi B tayari Netherlands na Chile
zimefuzu kuingia Raundi ya Pili lakini kinachopiganiwa ni nani atamaliza
Nambari Wani ili ‘kumkwepa Mwenyeji Brazil’ Mechi ijayo.
Wadau wengi wanaipa nafasi kubwa Brazil
kushinda Kundi A na hivyo kucheza na Mshindi wa Pili Kundi B na hilo
ndio motisha ya Mechi ya Netherlands na Chile.
IFUATAYO NI TATHMINI YA KUNDI KWA KUNDI:
KUNDI A |
||||||||
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
Brazil |
2 |
1 |
1 |
0 |
3 |
1 |
2 |
4 |
Mexico |
2 |
1 |
1 |
0 |
1 |
0 |
1 |
4 |
Croatia |
2 |
1 |
0 |
1 |
5 |
3 |
2 |
3 |
Cameroon |
2 |
0 |
0 |
2 |
0 |
5 |
-5 |
0 |
Mechi za Mwisho:
-Croatia v Mexico
-Cameroon v Brazil
Brazil na Mexico zinahitaji Sare tu kufuzu.
Lakini Brazil inaweza kufuzu hata ikifungwa na Cameroon ikiwa Mexico itaifunga Croatia.
Ili Croatia ifuzu inahitaji ushindi ingawa Sare inaweza kuwapitisha ikiwa tu Brazil itafungwa na Cameroon.
KUNDI B |
||||||||
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
Netherlands |
2 |
2 |
0 |
0 |
8 |
3 |
5 |
6 |
Chile |
2 |
2 |
0 |
0 |
5 |
1 |
4 |
6 |
Australia |
2 |
0 |
0 |
2 |
3 |
6 |
-3 |
0 |
Spain |
2 |
0 |
0 |
2 |
1 |
7 |
-6 |
0 |
Mechi za Mwisho:
-Australia v Spain
-Netherlands v Chile
Tayari Netherlands na Chile zimefuzu na Mechi kati yao itaamua nani Mshindi wa Kwanza wa Kundi.
Netherlands wanahitaji Sare tu wabaki kileleni.
KOMBE LA DUNIA
MECHI ZA MWISHO ZA KUNDI A na B:
JUMATATU, JUNI 23, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
Australia v Spain |
B |
Arena da Baixada |
1900 |
Netherlands v Chile |
B |
Arena Corinthians |
2300 |
Croatia v Mexico |
A |
Arena Pernambuco |
2300 |
Cameroon v Brazil |
A |
Nacional |
0 comments:
Post a Comment