Monday 23 June 2014

RONALDO AUNGAMA URENO SI WAZURI KUWA MABINGWA WA DUNIA!

>>NI ‘LAANA’ YA MCHEZAJI BORA DUNIANI KUTOTWAA KOMBE LA DUNIA MWAKA ANAOTWAA TUZO!!
RONALDO-AKIRIMCHEZAJI BORA DUNIANI Cristiano Ronaldo amekiri kuwa si Portugal wazuri wa kutwaa Kombe la Dunia.
Ronaldo aliungama mara baada ya Jana kutoka Sare 2-2 na USA huku yeye ndio akitoa Pasi murua iliyounganishwa kwa Kichwa na Silvestre Varela kwenye Sekunde za mwisho na kuwapa Droo ya 2-2 ambayo imeweka hai kidogo matumaini yao finyu ya kusonga Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Hata hivyo, Portugal, ambao walinyukwa Bao 4-0 na Germany kwenye Mechi yao ya kwanza ya Kundi G huko Brazil, ni lazima waifunge Ghana kwenye Mechi yao ya mwisho na pia kuomba kwenye Mechi ya Germany na USA mmoja afungwe kwa Bao nyingi tu ili wao, kama watapenya, iwe kwa ubora wa tofauti ya Magoli tu.
Lakini Ronaldo inaelekea amekubali ile ‘laana’ ya Kihistoria ya Mchezaji Bora Duniani kutochukua Kombe la Dunia Mwaka anaotwaa Tuzo hiyo.
Ronaldo ametamka: “Portugal haikupewa nafasi. Hata kufuzu kuja Fainali ilikuwa ni kazi kubwa!”
Ronaldo ndie alieifikisha Portugal Fainali hizi za Brazil baada ya kuibwaga Sweden kwa jumla ya Mabao 4-2 kwa Mechi mbili za Mchujo huku yeye akipiga Hetitriki katika Mechi ya Marudiano huko Stockholm waliyoshinda 3-2.
Ronaldo aliongeza: “Sikuwahi kufikiria tutakuwa Mabingwa wa Dunia. Lazima tuwe wakweli tukubali udhaifu wetu. Kwa sasa zipo Timu Bora na Wachezaji Bora kupita wetu.”

0 comments: