Monday 23 June 2014

MAJAMBAZI:WAVAMIA NA KUUWA (SISTER)KWA RISASI UBONGO DAR!! ANGALI TUKIO ZIMA HAPA.

 

UJAMBAZI DAR: Kuna taarifa kuwa majambazi yameua sista mmoja kwa risasi Riverside, Ubungo mchana huu wa leo , na sista mwingine afanikiwa kuwatoroka, dereva wao ajeruhiwa ; kuna jama, mashuhuda wamenitumia ujembe...!
"kama kuna mdau yuko karibu na tukio atujuze kinachoendelea tafadhari"...!

====== Updates ========

SISTA wa Parokia ya Makoka iliyopo Kibangu, Dar ameuawa na majambazi yaliyokuwa kwenye bodoboda wakati akiingia kwenye gari akitokea dukani eneo la River Side, Ubungo jijini Dar es Salaam hivi punde.

Kabla ya kuuawa sista huyo, dereva wake alipigwa risasi mkononi na majambazi hayo.

Alikuwa anapeleka pesa bank alikuwa kwe tax. Walipofika maeneo ya msikitini ndio wakavamiwa na hao watu wawili walikua kwe pikipiki wakapiga risasi kwa nyuma ya gari ikampata sister kwe kichwa na nyingine ikampata Dereva kwe kidole gumba kikachambuka kama mchicha.
Mwili wa mtawa ukiwa umefunikwa.

Risasi nyingine ikapigwa hewani watu wakaanza kukimbia ndo wale majambazi wakaingia ndani ya ile taxi na kuchukua pochi ya sister.


Dereva akionesha kidole gumba kilichopigwa risasi.

Ila walibugi stepu maana pesa hazikua kwe pochi zilikua kwe gari. Mungu ailaze pema roho ya sister na Dereva apone haraka ili arudi kazini salama.

CHANZO NA JF
  By Chachu Ombara  
 

0 comments: