BAADA YA KUIFUNGA ITALIA, MARADONA AWAWAKIA FIFA ILE MBAYA
GWIJI
Diego Maradona amewashambulia FIFA baada ya kuagiza wachezaji saba wa
Costa Rica wafanyiwe vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu
zilizokatazwa kufuatia kuifunga Italia.
Gwiji huyo wa soka Argentina amesema bodi hiyo ya kandanda duniani inaonyesha kutoheshimu sheria kwa agizo.
Wachezaji
wawili tu wa Italia walifanyiwa vipimo baada ya kip[igo cha 1-0 kutoka
kwa Costa Rica Ijumaa– na kuzima matumaini ya England kusonga mbele
kutoka kwenye makundi.
Maradona, mwenye umri wa miaka 53, amesema: "Kama kuna wachezaji saba wa Costa Rican, kwa nini haiku hivyo kwa Italia?
"Hii
ni mpya. Lakini hii inatokea kwa sababu imewaumiza mno watu kuona Costa
Rica inasonga mbele na hao mabingwa wa dunia hawajafuzu, kwa sababu
wadhamini hawatatoa fedha walizoahidi.
"Ni
kinyume cha sheria. Kila inatakiwa kupeleka wachezaji wawili kwa vipimo
vya dawa za kuongeza nguvu. Ilitokea kwangu, iliniumiza, hivyo nipo
tayari kuzungumzia mpango huu. Lakini wachezaji saba, haiwezekani.
"Kuchukua wachezaji saba wa Costa Ricans kwa vipimo vya dawa inaomyesha kutoheshimu wachezaji na sheria. Costa Rica imefuzu kishujaa, jape ilikuwa ina mabingwa watatu wa dunia kwenye kundi na imewafunga kwa soka nzuri,".
Mshituko: Costa Rica imeshinda mechi zake mbili za mwanzo dhidi ya Uruguay na Italy Kombe la Dunia
Maradona
alishinda Kombe la Dunia na Argentina mwaka 1986 lakini alirudishwa
nyumbani katika fainali za mwaka 1994 baada ya kugundulika alitmia dawa
aina ya ephedrine wakati wa vipimo. Pia aligundulika anatumia deawa za
kulebya aina ya cocaine mwaka 1991 na akafungiwa kwa miezi 15.
Ametoa maoni yake kupitia kipindi cha Televisheni ya Argentina, De Zurda. Gazeti la Costa
Rica liliwataja wachezaji saba waliofanyiwa vipimo hivyo kuwa ni Bryan
Ruiz, Michael Barrantes, Keylor Navas, Celso Borges, Christian Bolanos,
Marco Urena na Diego Calvo.
Gazeti
hilo, El Dia limesema vipimo hivyo vinaonyesha kwamba FIFA ina wasiwasi
nba Costa Rican baada ya kuzifunga Uruguay na Italia.
0 comments:
Post a Comment