Sunday 11 January 2015

EPL: SOTON WAVUNJA REKODI YA MIAKA 27 DHIDI YA MANCHESTER UNITED


Ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena jioni ya leo kwa michezo miwili kucheza katika viwanja tofauti nchini humo – moja ya mechi ilikuwa inawakutanisha timu zinazogombania kuendelea kuwemo kwenye 4 bora – Man United vs Southampton.
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford umeshuhudia rekodi ya miaka 27 ya Soton kutokuifunga Man United katika uwanja wa nyumbani kwenye EPL ikivunjika.
Goli la dakika ya 69 la Tadic limewapa Southampton ushindi ambao pia umewapandisha mpaka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.
Katika mchezo mwingine wa leo hii Arsenal waliifunga Stoke City 3-0 na kupanda hadi nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi.

0 comments: