Sunday 2 March 2014

ANGLIA PICHA 7 KUHUSU MAUAJI YALIYOTOKEA KWENYE KITUO CHA TRENI NCHINI CHINA

 
1 
Taarifa iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali inasema kuwa kuna kundi la watu waliokuwa na visu limewashambulia na kuua watu 28 huku zaidi ya 100 wakijeruhiwa katika kituo cha treni kilichopo mjini Kunming nchini China.
6 
Mashahidi wa tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji hao walivalia nguo nyeusi na kuwavamia abiria waliokuwa wakingojea treni na kuwakatakata huku wengine wakiwadunga visu wale hasa walioshindwa kukimbia kwa kasi.
3 
Polisi wamefanikiwa kuwauwa washambuliaji watano kati ya kumi waliofanya shambulio hilo,Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo,ulinzi bado umeimarishwa eneo la tukio.
2
4
5
7

0 comments: