Dar es Salaam. Upande wa
utetezi katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
(FFU) na mfanyakazi wa Benki ya NMB, maarufu mauaji ya Ubungo Mataa,
umepinga ripoti ya uchunguzi wa silaha zilizotumika katika mauaji hayo,
isipokewe mahakamani.
Upande wa mashtaka katika kesi hiyo (Jamhuri),
uliomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ipokee ripoti hiyo ambayo
ndiyo inayobainisha silaha zilizotumika katika mauaji hayo, ili iwe
kielelezo cha ushahidi cha upande wa mashtaka.
Jamhuri iliomba kuwasilisha ripoti hiyo kupitia
kwa shahidi wake wa 29, Mtaalamu wa milipuko, aliyefanya uchunguzi wa
silaha hizo zilizotumika katika tukio hilo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi,
Godfrey Luhamba.
Hata hivyo, Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Richard Rweyongeza, walipinga ripoti hiyo, wakidai utaratibu uliotumiwa na upande wa mashtaka ni kinyume cha sheria.
Akizungumza kwa niaba ya jopo la mawakili wa
utetezi, Wakili Rweyongeza alisema ripoti hiyo haikuwahi kusomwa kwa
washtakiwa hao, wakati wa uhamishaji shauri lao (Committal) kutoka
Kisutu kwenda Mahakama
CHANZO Kuu.Na James Magai,Mwananchi
CHANZO Kuu.Na James Magai,Mwananchi
0 comments:
Post a Comment