Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwa kushirikiana na
wananchi, wakimdhibiti mmoja wa vijana waliofanya fujo katika mkutano wa
hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Dk. Willibrod Slaa, uliofanyika katika kijiji cha Mabamba wilayani
Kibondo mkoani Kigoma. (Picha na Joseph Senga)
KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa
jana alitibua mkakati wa kuvuruga mkutano wake uliofanywa na vijana
watano kwa kutumia jina la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe,
baada ya kuwakaribisha wasogee mbele ya jukwaa ili awasikie vizuri.
Kabla ya hapo, Dk. Slaa alifanya kitendo kilichowashangaza wengi
mkutanoni, wakiwemo askari, baada ya kuwataka polisi waache mara moja
kuchana mabango ya vijana hao na wasiendelee kuwazuia kujitokeza mbele
ya mkutano wake uliofanyika jana mjini Kakonko.
“Polisi wangu nawaomba sana msiendelee kuchana mabango ya hao vijana wala msihangaike nao kuwazuia wasije hapa, tena ningependa kuwaona, waacheni wasogee hapa mbele ya watu wote.
“Chama hiki ni cha kidemokrasia, wala wasiwapatie taabu. Tunajua kuwa hayo yapo,” alisema Dk. Slaa.
Vijana hao walionekana wakitoa mabango yao mifukoni mara tu baada ya msafara wa Dk. Slaa kuwasili eneo la mkutano

ambapo
kiongozi huyo alifungua dirisha na akiwaonyesha ishara ya kuwaita eneo
la mkutano, huku akiwataka wasikae mbali na hayo madukuduku yao ili
waende kupata majibu kama wana maswali.
Akihutubia mkutano huo wa pili katika Uwanja wa Mwenge mjini Kakonko, akiwa ametokea kijiji cha Muhange, kata ya Muhange, ambako alifanya mkutano wake wa kwanza, Dk. Slaa alianza kwa kuwataka vijana hao wasogee mbele ya jukwaa ili wamsikie naye ayaone mabango yao yameandika nini.
“Vijana wangu hebu sogeeni hapa mbele kabisa ya jukwaa mkae hapa, kaeni hapa niwaone na nisome mlichoandika maana huko sioni mabango yenu yameandikwa nini,” alisema Dk. Slaa huku vijana hao wakitii amri hiyo.
“Najua watu wengi mlishangaa nilipowazuia wale polisi wangu wasiendelee kuwazuia hawa wasije hapa mkutanoni na wasichane mabango yao.
“Haya mambo tulijua kuwa yangelikuwepo. Hayatusumbui kabisa. Naomba wananchi wangu kama mlivyoshangilia muwasikitikie tu hawa vijana maana hawajui wanachokifanya. Hebu ngoja niwaulize vijana wangu.”

Dk.
Slaa alianza kuwauliza vijana hao masuala kuhusu CHADEMA, ambapo alitaka
kujua kama wanaifahamu katiba ya chama chao, nao walijibu mmoja mmoja
kuwa hawajui, kisha akawauliza kadi za chama, wakajibu pia mmojammoja
kuwa hawana, akawahoji tena kila mmoja aseme anatokea tawi gani.
Wakasema hawajui matawi yao, kisha akawauliza kama walikuwa wanawajua viongozi wa matawi yao, wakajibu walikuwa hawamjui kiongozi wao hata mmoja.
Kisha mmoja wao akasikika akisema, “Mimi ni mtoto wa mwenezi mstaafu wa CCM, sijui hayo mambo.”
“Vijana wangu ni wazi hamjui mnachokifanya. Mnatumika tu, ndiyo maana nilitaka mje hapa karibu yangu, maana najua hamjui kitu mnastahili kuhurumiwa na kusikitikiwa! “Haya nikiwaambia hawa askari hapa wakawapime kiwango cha pombe mlicholewa leo mchana nani kati yenu atasalimika hapa?
“Wote! Kila mmoja hapa anaweza kuona mlivyolewa! “Askari mnaweza kuwapima hawa…aah! Haya! Hamna vifaa…bahati yenu; wanasema hawana vifaa,” alisema Dk. Slaa huku vijana hao mmojammoja akianza kuondoka jukwaani wakikunja mabango yao, huku wananchi wakiwazomea kwa nguvu, wakiwaita ombaomba.

Baada
ya kuondoka mbele ya jukwaa, vijana hao waligawanyika ambapo watatu
waliondoka kabisa eneo la mkutano na kuwaacha wenzao wawili wakiwa
wamekunja mabango yao.
Mabango hayo ambayo yalionekana kuandikwa kwa hati moja ya mwandiko, yalisomeka hivi: “Tanzania, Kigoma, Kakonko bila Zitto haiwezekani; Mhe. Slaa, Mhe. Mbowe wote wajiuzulu mara moja; Hatuko tayari kusikiliza lolote bila Zitto.”
Baada ya vijana hao kuondoka kwa kunyongea, Dk. Slaa akishangiliwa na umati wa watu, aliendelea kuhutubia ambapo alisema ziara yake mkoani Kigoma haina uhusiano na masuala ya tuhuma za utovu wa nidhamu na uvunjwaji wa misingi ya chama hicho yanayoendelea ndani ya chama hicho, akisema kuwa ziara hiyo ilipangwa tangu Julai mwaka huu.
Alizidi kueleza kuwa ziara hiyo iliahirishwa mara tatu kutokana na majukumu ya kichama aliyokuwa akiyapata ndani na nje ya nchi, lakini akaendelea kupata msisitizo kutoka kwa viongozi hasa wa wilaya za Kasulu na Kibondo, kutokana na manyanyaso ambayo wananchi wanayapata kutoka kwa viongozi wa serikali na vyombo vya dola.
“Nimewauliza vijana wale masuala ambayo mwana CHADEMA yeyote anapaswa kuyafahamu na kuyajua, mambo yote yanayoendesha CHADEMA yamo ndani ya kitabu hiki. Kitabu cha katiba kina sehemu ya maadili, kanuni, itifaki pia tunayo miongozo ya chama. Si Mbowe, si Dk. Slaa, wala Mzee Mtei muasisi wa chama anaweza kuwa juu ya kitabu hiki.
“Ni kama ilivyo kwa Muislamu safi hawezi kuwa juu ya Korani au Mkristo hawezi kuwa juu ya Biblia. Hakuna! Ndugu zangu chama hiki kimekuwa kikubwa mno, si chama cha mtu yeyote yule, hakiendeshwi kwa kauli ya Mbowe, Slaa wala mtu mwingine. Hakuna aliye juu ya katiba hii. Kama kuna mtu hayuko tayari!”
via Tanzania daima

Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod
Slaa, akipokea kadi ya uanachama, kutoka kwa liyekuwa Mwenyekiti
Kitongoji cha Mtaa wa Shule katika Kijiji cha Mabamba kupitia CCM,
Sevelino Damian, ambaye amehemia Chadema, wakati wa mktano wa hadhara
uliofanyika kijijini hapo.
0 comments:
Post a Comment