Saturday, 7 December 2013

LEO OLD TRAFFORD MOTO, MOYES ATAKA JIBU BAADA KIPIGO!!

NI MAN UNITED v NEWCASTLE BILA ROONEY & RVP!!
 LEO PIA SOUTHAMPTON v MAN CITY, STOKE v CHELSEA!!
 JUMAPILI: ARSENAL v EVERTON!!
BPL2013LOGODavid Moyes ametaka Manchester United isimamishe kupotea kwa Msimu wao wakati leo wakikabiliana na Newcastle Uwanjani Old Trafford.
Juzi Jumatano, wakiwa hapo hapo Old Trafford, Man United walijikuta wakichapwa Bao 1-0 na Everton kwa Bao la Dakika ya 86.
Kipigo hicho kiliwaacha Man United wakielea Nafasi ya 9 Pointi 12 nyuma ya Vinara wa Ligi Arsenal.
Kipigo hicho ni balaa jingine kwa David Moyes ambae amemrithi Sir Alex Ferguson Msimu huu kwani tayari washapokea vichapo vinne Msimu huu baada Mechi 14 wakati Msimu uliopita katika Mechi zote 38 walifungwa mara 5 tu.
Hata hivyo, Moyes bado ana imani Man United watafanya vyema ikiwa watajinusuru mapema.
Akiongea na MUTV, TV ya Man United, Moyes alisema: “Nimesikitishwa lakini tunaendelea tena na Gemu nyingine. Hatukufikia malengo yetu na Everton. Lakini huku zipo Gemu nyingi na tunaendelea.”
Nae Meneja wa Newcastle, Alan Pardew, anaamini Moyes atapata majibu sahihi hivi karibuni.
Lakini Man United leo ina tatizo kubwa kwani itawakosa Nyota wao wakubwa wawili, Wayne Rooney, ambae yupo Kifungoni Mechi 1 baada kuzoa Kadi za Njano 5, na Robin van Persie ambae huenda asicheze kwa vile anakabiliwa na maumivu ya Nyonga.
Kusuasua kwa Mabingwa Man United kumeleta matumaini kwa Arsenal kupaa kileleni baada kuifunga Bao 2-0 Hull City na Jumapili wako kwao kucheza na Everton.
Leo Jumamosi, Chelsea wanasafiri kwenda kucheza na Stoke City na Manchester City, wakiwa Pointi 6 nyuma ya Arsenal na walio Nafasi ya Tatu, wanakwenda kucheza Ugenini na Southampton ambao wameporomoka hadi Nafasi ya 8 baada ya vipigo vitatu mfululizo.
Liverpool, ambao wako Nafasi ya 4, watakuwa Wenyeji wa West Ham na watataka ushindi mwingine mkubwa baada ya kuifumua Norwich City Bao 5-1 katika Mechi iliyopita ambayo Straika wao Luis Suarez alipiga Bao 4.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi Desemba 7
1545 Man United v Newcastle
1800 Crystal Palace v Cardiff
1800 Liverpool v West Ham
1800 Southampton v Man City
1800 Stoke v Chelsea
1800 West Brom v Norwich
2030 Sunderland v Tottenham
Jumapili Desemba 8
1630 Fulham v Aston Villa
1900 Arsenal v Everton
Jumatatu Desemba 9
2300 Swansea v Hull
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
14
19
34
2
Chelsea
14
14
30
3
Man City
14
26
28
4
Liverpool
14
13
27
5
Everton
14
9
27
6
Tottenham
14
-2
24
7
Newcastle
14
-2
23
8
Southampton
14
5
22
9
Man Utd
14
4
22
10
Aston Villa
14
0
19
11
Swansea
14
1
18
12
Hull
14
-6
17
13
West Brom
14
-2
15
14
Stoke
14
-6
14
15
Cardiff
14
-9
14
16
Norwich
14
-16
14
17
West Ham
14
-3
13
18
Fulham
14
-14
10
19
Crystal Palace
14
-14
10
20
Sunderland
14
-17
8

0 comments: