Wednesday, 1 January 2014

MAPINDUZI CUP 2014:SIMBA SC YAITAFUNA LEOPARD 1-0, KMKM YALIZWA, MBEYA CITY YATOA SARE

 
blogger-image--1657134963
Amri Kiemba amewaliza AFC 

BAO pekee la kiungo mtata wa Wekundu wa Msimbazi, Simba sc, Amri Ramadhan Kiemba limetosha kuibuka na pointi 3 muhimu za kwanza usiku huu katika mechi yao ya kwanza  kombe la Mapinduzi 2014 iliyoanza kutimua vumbi leo hii viwanja viwili vya Amaan, Unguja na Gombani, Pemba.
Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa kocha wa Timu ya Taifa ya  Italia, Cesare Prandelli ambaye alikagua timu zote na kwenda katikati ya dimba la Amaan na kuudunda mpira ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa michuano ya mwaka huu.
Mchezo huo wa kundi B ulioanza majira ya saa 2:00 usiku ndio uliochaguliwa kuwa wa ufunguzi katika michuano ya mwaka huu ambayo ni maalumu kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Fundi Kiemba aliyeanzia benchi leo hii na kuingia dakika ya 47 kuchukua nafasi ya Kiungo mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar dirisha dogo mwaka jana, Awadh Juma Issa, alifunga bao hilo baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na beki wa AFC Leopard kufuatia Amisi Tambwe kujaribu kuunganisha krosi maridadi uliochongwa na Ramadhan Singano `Messi` dakika ya 77 ya mchezo.
`Messi` huyu mtoto ni nuksi tupu!, alifanya vitu vyake vya Nani Mtani Jembe baada ya kumlamba chenga ya aibu beki mrefu zaidi na mkongwe, Joseph Shikokoti na kupiga krosi iliyosababisha bao hilo muhimu.
Ushindi wa leo kwa Simba sc umewapatia nguvu zaidi katika harakati zao za kuusaka ubingwa ambao kwa mara ya mwisho kuutwaa ni mwaka 2011.
Kwasasa Azam fc ndio mabingwa watetezi mara mbili mfululizo, yaani walitwaa `ndoo` hiyo 2012 na 2013.
Hata hivyo imekuwa neema kwa kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola `Veron` ambaye alisimama kwenye benchi la ufundi wakati akimsubiri bosi wake Mcroatia, Zdravko Logarusic ambaye atawasili kesho Zanzibar.
Mechi ya leo ilijigawa kwa timu zote kwani Leopard walicheza vizuri dakika 45 za kwanza, lakini Simba SC walichachamaa kipindi cha pili na kucheza soka safi, lakini kukosa umakini kwa washambuliaji wa klabu hiyo kumewanyima ushindi mnono.
Simba sasa wanashika nafasi ya pili kundi B wakijikusanyia pointi tatu sawa na KCC ya Uganda wenye pointi 3, lakini wao wanawastani mzuri wa mabao ya kufunga.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rid, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Ramadhani Chombo/Uhuru Suleiman dk89, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk81, Ramadhan Singano, Awadhi Juma/Amri Kiemba dk47.
AFC Leopard; Martin Masalia, Etenesy Augustin, Abdallah Juma, Saleh Jackson, Joseph Shikokoti, Imbalebala Martin, Okwemba Charles, Mussa Mude, Kelly Jacb, Mang’ole Benard/Seda Edwin dk86 na Oscar Kadenge/Hassan Mohamed dk86.
Awali katika dimba hilo, mabingwa wa Zanzibar KMKM walilala kwa mabao 3-2 dhidi ya KCC kutoka nchini Uganda katika mchezo wa Kundi A.
Mabao ya KCC yalifungwa na Herman Waswa dakika ya 10, Tony Odur katika dakika ya 20 na William Waoro dakika ya 82, wakati ya KMKM yalifungwa na Hamisi Ali dakika ya saba na Maulid Ibrahim dakika ya 79.
Huko uwanja wa Gombani, Pemba, vijana wa Juma Mwabusi, Mbeya City wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Clove Stars. 
Bao la Mbeya City lilifungwa dakika ya 13 na Deus Kaseke, lakini dakika ya 24 kipindi hicho cha kwanza, Clove Stars Wakarudisha

0 comments: