MAJANGA yatokea mwaka mpya mkoa wa Iringa baada ya dereva boda
boda mmoja mjini Iringa kuvunjika mguu na abiria wake kujeruhiwa
vibaya wakati wakisherekea mwaka mpya 2014.
Majanga hayo yametokea usiku wa january 1 mwaka 2014 ikiwa ni
dakika 20 baada ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa dereva boda boda huyo akiwa
katika mwendo mkali na abiria wake walikuwa wakitokea mjini Iringa
kuelekea Ilala na baada ya kufika eneo la Mlyuka walijikuta
wakipata majanga haya baada ya gari aina ya Tx yenye namba T 397
AEZ kuhama upande wake na kuwavaa watu hao ambao walikuwa katika
boda boda.
mashuhuda hao walisema kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 6.20
usiku wa kuamkia leo na kuwa canhazo cha ajali hiyo ni dereva wa
taxi hiyo ambayo pia alikuwa katika harakati za kusherekea mwaka 2014
.
Akizungumza kwa shida akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Iringa dereva wa boda boda hiyo Bw Joseph Nyogele alisema kuwa
akiwa katika harakati za kuikwepa Taxi hiyo alijikuta akigongwana
kuvunjika mguu wake wa kushoto huku abiria wake akipoteza fahamu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kuwa mbali ya ajali hiyo wakati wa mkoa
wa Iringa wameuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014 kwa amani
na utulivu na kuwa hakuna vurugu zilizojitokeza wakati wa mkesha
huo .
Alisema kuwa wananchi waliheshimu agizo la jeshi la polisi katika
kuwataka kutofanya vurugu na kuwa hakuna vurugu zilizojitokeza na
hakuna eneo ambalo wananchi walichoma mataili .
Afisa muunguzi wa zamu katika Hospital hiyo ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa Eda Sanga alisema kuwa mwendesha boda boda huyo Nyogele
alivunjika mguu wake wa kushoto na kuwa mguu huo umekatwa na sasa
hali yake inaendelea vema huku abiria wake ametibiwa na kuruhusiwa .
wakati huo huo Sanga alisema kuwa jumla ya watoto 13 wamezaliwa
wakati wa mkesha wa mwaka mpya na kuwa kati ya watoto hao 7 ni wa
kiume na watano wa kike na watoto watatu kati yao wamezaliwa kwa njia
ya upasuaji na mama zao wanaendelea vizuri .
|
0 comments:
Post a Comment