KUWAKOSA WOTE ROONEY NA VAN PERSIE
MABINGWA
MANCHESTER UNITED huenda wakacheza Mechi ya Mwaka mpya dhidi ya
Tottenham bila ya Mastraika wao wakubwa kwa mara nyingine tena kama
alivyotoboa Meneja wao David Mpyes.
Robin van Persie amekuwa nje ya Uwanja
kwa Mechi 5 sasa akijiuguza Paja lake na Wayne Rooney aliikosa Mechi ya
Jumamosi walipoifunga Norwich City Bao 1-0 akiwa na tatizo la Nyonga.
Ingawa Robin van Persie ameshaanza tena
Mazoezi lakini Mechi hii na Tottenham Jumatano Usiku Uwanjani Old
Trafford huenda ni mapema mno kwake wakati Rooney atasubiri apimwe
Dakika za mwisho kabla ya Mechi ili kuthibitisha kama yuko fiti kabisa.
Akiongea na Wanahabari katika Mahojiano
maalum kabla ya pambano na Tottenham, David Moyes alisema: “Inabidi
tusubiri na kuona kuhusu Wayne. Hakufanya Mazoezi Jumatatu hivyo inabidi
tutathmini na tujue hali iko vipi. Robin bado hajawa tayari lakini
tunategemea hayuko mbali sana.”
Kukosekana kwa Mastraika hao wawili
kutafanya Danny Welbeck, ambae ndie alifunga Bao la ushindi huko Carrow
Road dhidi ya Norwich, na Javier Hernandez ‘Chicharito’ wawe na jukumu
la kuipa Man United ushindi wao wa 7 mfululizo lakini David Moyes
amepoza matumaini makubwa ya kuibuka upya.
Amesema: “Sidhani kama kuna Mtu
anajirusharusha kwa furaha kwa sababu tumeshinda Mechi 6 mfululizo-hapa
ni kitu kinachotegemewa!”
Aliongeza: “Tottenham ni wapinzani wagumu! Siku zote ni Timu nzuri na ngumu!”
Kwa sasa Tottenham inaongozwa na Tim
Sherwood baada ya kutimuliwa Andre Villas-Boas hapo Desemba 16 na tangu
wakati huo, Sherwood amemudu kuiongoza Tottenham kuifunga Southampton
3-2, Sare na West Brom na ushindi dhidi ya Stoke City.
Hivi sasa Tottenham wako nyuma tu ya Man United kwenye Msimamo wakiwa na Pointi sawa lakini wamezidiwa kwa ubora wa Magoli.
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham
0 comments:
Post a Comment