Wednesday, 1 January 2014

DREVA AKAMATWA AKIENDESHA GARI AKIWA AMELEWA

— Hivi karibuni Polisi na SUMATRA walifanya zoezi la kupima ulevi kwa madereva Chalinze, Mkoa wa Pwani.

Zoezi hilo lililokuwa linalenga kukipima ulevi kwa madereva wa usafirishaji hasa kwa mabasi yaendayo mikoani, lilikuwa na lengo la kukamata madereva waliokunywa pombe na kuendesha magari hivyo kuhatarisha usalama wa abiria, wao binafsi na watumiaji wengine wa barabara.
Hatimaye zoezi hilo lilikuwa na mafanikio baada ya madereva kadhaa kukamatwa wakiwa wamekunywa pombe na
baadhi walipoulizwa walisema walikunywa pombe waliyoiita viroba.

Dereva huyo alibainika kuwa alikuwa amelewa kutokana na vipimo kutoka kwa police wa usalama Barabarani.

Polisi ililazimika kulizuia gari hilo na kumshikilia dereva huyo ambaye hakutaka kutaja jina alipoulizwa. Police kwa kushirikiana na maofisa wa SUMATRA waliwasilina na mmiliki wa mabasi hayo ili aleta dereva mwingine na hatimaye abiria kuendelea na safari yao.

Pongezi nyingi sana kwa SUMATRA na Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri ya kuokoa maisha ya Watanzania.

 
Via Imma Matukio blog

0 comments: