Wednesday, 1 January 2014

UN: VITA VISITISHWE SUDANI KUSINI ILI KULETA AMANI NCHINI HUMO

Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka makwao kutokana na vita kutokota
Mkuu wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini humo.
Hilde Johnson aliyeelezea wasiwasi wa hali mbaya ya kibinadamu nchini humo, amezitaka pande zinazozozana kukubali kufanya mazungumzo ya amani.
CHANZO BBCSWAHILI

0 comments: