Kiwanda cha ngozi kilichopo manispaa ya Shinyanga ambacho kimekamilika na kazi ya kujaribisha mitambo inaendelea.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Ally N.Rufunga akipata maelezo ya maendeleo ya kiwanda hicho alipotembelea ili kuona shughuli zinazoendelea.
Mashine za kuosha na kulainisha ngozi zikijaribiwa, chini ni ngozi zinazosubiri kuwekwa kwenye mashine hizo.
Mkuu
wa Mkoa akioneshwa baada ya kazi ngozi laini inavyokuwa na tayari kwa
matumizi mbalimbali kama kutengeneza viatu,mabegi,pochi,n.k
Hizi ni mashine za kutengeneza yuzi katika kiwanda cha nyuzi na nguo kilichopo manispaa ya Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa Mhe. Ally N. Rufunga akiona shughuli ya kujaribu mitambo katika
kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong leo alipotembelea kiwanda hicho.
Ndani
ya kiwanda cha kukamua mafuta cha Jielong ambapo Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Mhe.Ally N. Rufunga amekitembelea mapema leo na kujionea kazi
ya kujaribu mitambo.
Kiwanda
cha kutengeneza Ngozi kwa ajili ya matumizi mbalimbali cha kampuni ya
Kichina “Xiu hua” kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga mkoani
Shinyanga kimekamilika ambapo mhandisi na msimamizi wa kiwanda hicho
“Mr.Way” amesema kwa sasa majaribio yanafanyika kabla ya kuanza
uzalishaji wakati wowote.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametembelea kiwanda hicho
mapema leo na kujionea majaribio ya mitambo ya kutengeneza ngozi za
mbuzi,kondoo na ng’ombe.
Kiwanda
hicho kinachotarajiwa kutengeneza jumla ya ngozi za kondoo na mbuzi
Elfu kumi hadi 12 kwa siku na ngozi za ng’ombe 2500, kitaajiri zaidi ya
Watanzania 500 ambapo Mr.Way amesema kipaumbele zaidi ni kwa wakazi wa
mkoa wa Shinyanga.
Mkuu
wa Mkoa pia ametembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya pamba cha Jielong
Holdings, ameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho Mr. Jerry Q
kuwa wanaendelea kuzifanyia majaribio mashine na wakati wowote kitaanza
kazi ya uzalishaji.
Mr.Jerry amesema kitaajiri zaidi ya wananchi 180 kitakapoanza uzalishaji na tayari kimeanza kuajiri.
Aidha,kiwanda
cha kutengeneza nyuzi za nguo cha Dahong ambacho kinatarajiwa kuanza
kazi mapema mwezi Machi baada ya kukamilisha kazi ya kufunga mashine
mwishoni mwa mwezi Februari.
Msimamizi wa kiwanda hicho Mr.Saimon amesema kiwanda hicho kitaajiri wananchi zaidi ya 80.
Mhe.Rufunga
amefanya ziara hiyo ili kujua maendeleo ya viwanda hivyo ambavyo
vinatarajiwa vitakapokamilika pamoja na viwanda vingine, vitabadili sura
ya mkoa wa Shinyanga kimaendeleo kwa kukuza uchumi wa mkoa,kwani
amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maisha ya wananchi wa Shinyanga
yanabadilika kwa kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vitakavyozalisha
ajira nyingi zitakazonufaisha wananchi.
0 comments:
Post a Comment