Rais wa muda wa Misri, Adly Mansour, amesema uchaguzi wa rais utafanywa kwanza kabla ya uchaguzi wa bunge.
Hayo ni mabadiliko ya utaratibu uliokubaliwa
baada ya rais wa Muslim Brotherhood, Mohamed Morsi, kuondolewa
madarakani mwaka jana.
Jumamosi, maelfu ya watu walikusanyika katika medani ya Tahrir mjini Cairo katika siku ya kuadhimisha miaka mitatu tangu Hosni Mubarak kupinduliwa.
Umati huo ulimtaka Jenerali al-Sisi agombee uongozi.
Wakati huohuo wakuu wamesema watu kama 49 waliuwawa katika sehemu mbali-mbali za nchi, wakati askari wa usalama walipopambana na waandamanaji wanaopinga serikali.
0 comments:
Post a Comment