Moja
kati ya familia maarufu hivi sasa kwenye kiwanda cha burudani ni ya Mr
and Mrs Carter ambao wote wawili wana-status kubwa kwenye muziki.
Mwaka jana wote wawili walitoka na vitu vipya kwenye soko la muziki kwa kuanza kuuza album zao kwa njia tofauti kabisa.
Jay Z alitoa album yake ya Magna carta holy grail kupitia app ya
Samsung na Beyonce alitoa ghafla bila hata promotion album yake kupitia
iTunes.
Mambo haya na mengine mengi kama kushinda tuzo,tours, kukusanya
mashabiki wengi,ushawishi kwenye game ya muziki,mikataba na makampuni
mbalimbali imeshawishi Billboard Magazine kuwataja kama most powerful
couples kwenye muziki.
Unadhani kwa Tanzania most powerful couple kwenye kiwanda chote cha
burudani(muziki.michezo,movie na vingine) watakuwa nani na nani?
0 comments:
Post a Comment