>>NI ZIMBABWE v LIBYA, GHANA v NIGERIA!!
ROBO FAINALI
MATOKEO:
Jumapili Januari 26
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
Ghana 1 Congo DR 0
Kwenye Mechi ya Awali, Dakika 90 za Robo
Fainali kati ya Gabon na Libya ilimalizika kwa suluhu ya 1-1 baada
Libya kutangulia kufunga katika Dakika ya 50 kupitia Abdelsalam Omar na
Daniel Cousin kuisawazishia Gabon Dakika ya 74 kwa Penati baada ya
Fetori kumvuta Lionel Yackouya na Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30
bila mabadiliko.
Kwenye Mikwaju ya Penati, baada Dakika
120, Libya walitoka Washindi kwa Penati 4-2 baada kufunga Penati zao
zote 4 na Gabon kukosa 2 na kutinga Nusu Fainali ambapo Jumatano
watacheza na Zimbabwe.
Katika Mechi iliyofuatia, Penati ya
Dakika ya 68 ya Kwabina Adusei imewapeleka Ghana Nusu Fainali baada ya
kuifunga Congo DR Bao 1-0.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Kimwika wa Congo DR kuunawa Mpira kwenye Boksi.
Kwenye Nusu Fainali Jumatano ijayo, Ghana watawavaa Wapinzani wao wa Jadi Nigeria.
VIKOSI:
Ghana: Adams; Adusei
(Azumah 70’), Ainooson, Sulley, Tijani; Akuffo (Owusu 82’), Mpong
(Attorbah 53’), Opoku; Mohammed, Anobaah, Bansey
Congo DR: Kidiaba;
Litombe, Kasusula, Muselenge, Kimwaki; Nsimbi, Ndombe (Mukanisa 85’),
Basisila (Emomo 72’), Mundele; Mabidi, Mavuanga (Nzinga 63’)
ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
[Cape Town Stadium]
Morocco 3 Nigeria 4 [3-3 baada Dakika 90]
Mali 1 Zimbabwe 2
Jumapili Januari 26
[SAA za Bongo]
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
Ghana 1 Congo DR 0
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
[SAA za Bongo]
1800 Zimbabwe v Libya [Free State Stadium]
2130 Ghana v Nigeria [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
[SAA za Bongo]
1800 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
2100 Fainali [Cape Town Stadium]
0 comments:
Post a Comment