Serikali ya Sudan Kusini
imewashutumu waasi kuwa wamevunja makubaliano ya kusitisha mapigano, saa
chache baada ya mkataba kuanza kutekelezwa.
Waziri wa habari, Michael Makuei Leuth, alisema
maeneo ya serikali bado yanashambuliwa na alionya kuwa serikali huenda
ikalazimika kujihami.Pande hizo mbili katika vita vya Sudan Kusini zimekubaliana kusitisha mapigano kumaliza mapambano ya wiki tano ambayo yameuwa maelfu ya watu.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yalitiwa saini Alkhamisis, lakini yalianza kutekelezwa saa 24 baadae.
Waziri Lueth hakueleza mapigano hayo yanatokea wapi nchini, lakini kulikuwa na mapambano Ijumaa katika jimbo la Jonglei.
0 comments:
Post a Comment