Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Hassan Tati akikagua mashamba
ya mazao mbali mbali yaliyoharibiwa na mvua kubwa ya mawe na upepo mkali
iliyonyesha juzi katika kijiji cha Siuyu.Jumla la ekari zai ya 800
zilimeharibiwa na mvua hiyo.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi
ZAIDI
ya ekari 800 za mazao mbalimbali yaliyolimwa katika vitongoji vinne vya
kijiji cha Siuyu tarafa ya Mungaa wilaya ya Ikungi,zimeharibiwa vibaya
na mvua kubwa ya mawe na iliyoambatana na upepo mkali.
Hayo
yamesemwa hivi karibuni na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Unyankhanya
wilaya ya Ikungi,Adriano Herman wakati akitoa taarifa ya uharibifu
mkubwa wa mazao kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tati.
Amesema mvua hiyo iliyonyesha juzi usiku kuanzia saa 1.30 jioni hadi saa 2.48 usiku pia ilisababisha nyumba tatu kuanguka chini.
“Mvua
hii ilionyesha mapema kwamba sio ya kheri kutokana na upepo wake kuwa
mkali mno.Pia ilidondosha mabonge makubwa ya barafu ambayo yalichukua
siku nzima kuyeyuka.Kwa ujumla imeharibu ekari 843,213 ya mazao
mbalimbali”,amesema.
Herman
alitaja mazao yaliyoharibiwa na ekari zake kwenye mabano kuwa ni viazi
vitamu (12),mtama (262),uwele (93),alizeti (37.5),maharage
(92.5),mahindi (137),ulezsi (201.5) na karanga (7.5).
Pamoja
na kuwapa pole wakazi hao,Mwenyekiti Tati aliwahakikishia kuwa
halmashauri ya wilaya ya Ikungi,inafanya maandalizi ya kuwasaidia mbegu
bora za mazao yanayokomaa kwa muda mfupi.
Aidha, Tati amewataka kuendelea kufuata masharti na ushauri wa watalaam wa kilimo ili waweze kupata mavuno ya kukidhi mahitaji.
“Nitumie
fursa hii kuwakumbusha wakulima wote wa wilaya ya Ikungi,kuhakikisha
wanalima mazao ya chakula na biashara yaliyopewa kipaumbele na mkoa
wetu”,amesema mwenyekiti huyo wa CCM.
0 comments:
Post a Comment