SOMA ZAIDI:
WEST HAM KUMKATIA RUFAA CARROLL!
WEST HAM imeijulisha FA nia yao ya
kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao Andy Carroll aliyopewa
Juzi Jumamosi walipoifunga Swansea City.
Carroll alipewa Kadi Nyekundu na Refa Howard Webb baada kugongana na Beki wa Swansea, Chico Flores.
West Ham walikuwa na nafasi hadi hii leo
Saa 10 Jioni, Bongo Taimu, kuwajulisha FA nia yao kama wanataka kupinga
Kadi hiyo na baada kufanya hivyo taratibu zinawapa Masaa mengine 24 ya
kutayarisha na kuwasilisha Ushahidi wao kuipinga Kadi Nyekundu hiyo.
Juzi,mara baada ya Mechi, Meneja wa West
Ham Sam Allardyce alimlaani Chico Flores kwa kusababisha Andy Carroll
atolewe na kudai wataikatia Rufaa Kadi hiyo.
Baada West Ham kukata Rufaa, Jopo Huru
la Watu Watatu litakaa na kupitia ushahidi wa pande zote, Marefa na West
Ham, na pia kuangalia Mkanda wa Video wa Tukio lenyewe na kisha kutoa
uamuzi.
Ikiwa Rufaa itatupwa nje, Carroll
atatumikia Kifungo cha Mechi 3 na kuzikosa Mechi za Timu yake dhidi ya
Aston Villa, Norwich na Southampton.
Mechi hiyo na Swansea ilikuwa Mechi ya 3
tu kwa Carroll kurudi Uwanjani baada kuwa Majeruhi kwa karibu Miezi 8
na ni yeye ndie alietengeneza Bao zote mbili zilizofungwa na Kevin Nolan
walipoichapa Swansea Bao 2-0.
MATA ADAI GUNDU LITAISHA!
Mchezaji mpya wa Mabingwa Manchester United, Juan Mata, amedai bahati mbaya iliyowasakama itaisha hivi karibuni.
Juzi Man United walikikwaa kipigo cha 8
kwenye Ligi Kuu England walipofungwa 2-1 na Stoke City huku Robin van
Persie, Wayne Rooney na Mata wakianza Mechi ya kwanza pamoja kwa mara ya
kwanza.
Lakini Mata anaamini bahati mbaya
itaisha na amesema: “Bahati mbaya hatukushinda Mechi yetu ya pili Wiki
hiyo. Ni Uwanja mgumu na upepo mkali haukusaidia kucheza Soka. Lakini
hatukustahili kufungwa!”
Aliongeza: “Tulikuwa na bahati mbaya kwa
Goli lao la kwanza, tukarudisha na tulijua tutashinda lakini tukafungwa
la pili kwa Bao la bahati pia. Tulipata nafasi nzuri hatukuzitumia.
Lakini tunahisi hatuwezi kufungwa tena Gemu kama hizi. Natumai ile
bahati iliyotoweka kwetu itarudi tena kwani tuna bahati mbaya hata
kwenye Majeruhi. Tulipoteza Masentahafu wawili kabla Haftaimu. Lakini
naamini tutaanza mbio za ushindi na kuwa bora zaidi!”
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
24 |
26 |
55 |
2 |
Man City |
23 |
42 |
53 |
3 |
Chelsea |
23 |
23 |
50 |
4 |
Liverpool |
24 |
29 |
47 |
5 |
Everton |
24 |
12 |
45 |
6 |
Tottenham |
24 |
-1 |
44 |
7 |
Man Utd |
24 |
10 |
40 |
8 |
Newcastle |
24 |
1 |
37 |
9 |
Southampton |
24 |
7 |
35 |
10 |
Aston Villa |
24 |
-7 |
27 |
11 |
Stoke |
24 |
-14 |
25 |
12 |
Swansea |
24 |
-6 |
24 |
13 |
Hull |
24 |
-7 |
24 |
14 |
Sunderland |
24 |
-11 |
24 |
15 |
Norwich |
24 |
-18 |
24 |
16 |
Crystal Palace |
24 |
-18 |
23 |
17 |
West Brom |
24 |
-6 |
23 |
18 |
West Ham |
24 |
-9 |
22 |
19 |
Cardiff |
24 |
-22 |
21 |
20 |
Fulham |
24 |
-31 |
19 |
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 8
1545 Liverpool v Arsenal
1800 Aston Villa v West Ham
1800 Chelsea v Newcastle
1800C rystal Palace v West Brom
1800 Norwich v Man City
1800 Southampton v Stoke
1800 Sunderland v Hull
2030 Swansea v Cardiff
Jumapili Februari 9
1630 Tottenham v Everton
1900 Man United v Fulham
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man Unitwd
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool
0 comments:
Post a Comment