Saturday, 22 February 2014

VPL: YANGA YAFUMUA RUVU SHO OTING7-0,NA COASTAL UNION YAICHAPA MBEYA CITY 2-0!


Ligi Kuu Vodacom
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 22
Ruvu Shooting 0 Yanga 7
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union 2 Mbeya City 0
Oljoro JKT v Mgambo JKT
**MATOKEO MENGINE TUTALETA BAADAE

MABINGWA Watetezi wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wameitandika Ruvu Shooting Bao 7-0 na kukamata uongozi wa Ligi.
Yanga, wakimchezesha kwa mara ya kwanza Straika kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, walikuwa mbele kwa Bao 4-0 hadi Mapumziko huku Bao la Kwanza likifungwa na Didier Kavumbagu ndani ya Sekunde 40 tu tangu Mechi ianze.
Yanga walipata Bao la Pili katika Dakika ya pili tu Mfungaji akiwa Simon Msuva na Emmanuel Okwi kufungua akaunti yake ya Magoli ya Ligi kwa Yanga katika Dakika ya 27 alipopiga Bao la 3.
Mrisho Ngassa alifunga Bao la 4 Dakika ya 30 na hadi Haftaimu Yanga walikuwa mbele 4-0.
Kipindi cha Pili Yanga waliongeza Bao 3 kupitia Kavumbagu, Msuva na Kiiza.
Huko Mkwakwani Jijini Tanga, Coastal Union waliichapa Mbeya City Bao 2-0 kwa Bao za Chipukizi Mohamed Miraji aliefunga katika Dakika ya 80 na 92
VIKOSI:
YANGA: Deogratias Munish, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub,  Kelvin Yondani,  Frank Domayo, Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza
Akiba: Juma Kaseja, Juma Abdul, David Luhende, Rajab Zahir,  Athuman Idd, Hassan Dilunga, Said Bahanuzi
RUVU SHOOTING: Abdallah Ramadhani, Michael Aidan, Stephano Mwasyika, Mangasini Mbonosi, Shaaban, Ali Khan, Hamisi Ismail, Juma Nade, Elias Maguli, Jerome Lambele, Cosmas Lewis
Ligi Kuu Vodacom
RATIBA:
Jumapili Februari 23
Simba v JKT Ruvu
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumatano Februari 26
Azam FC v Ashanti United
MSIMAMO:
NA TIMU P W D L GD PTS
1 Yanga SC 17 11 5 1 29 38
2 Azam FC 16 10 6 0 19 36
3 Mbeya City 19 9 8 2 8 35
4 Simba SC 18 8 8 2 17 32
5 Coastal Union 19 5 10 4 5 25
6 Ruvu Shooting 18 6 7 5 -4 25
7 Kagera Sugar 18 5 8 5 0 23
8 Mtibwa Sugar 18 5 7 6 -1 22
9 JKT Ruvu 18 6 1 11 -14 19
10 Prisons FC 16 3 7 6 -3 16
11 Mgambo JKT 18 3 5 10 -18 14
12 Ashanti UTD 17 3 5 9 -14 14
13 JKT Oljoro 18 2 8 8 -14 14
14 Rhino Rangers 18 2 7 9 -10 13

0 comments: