Manchester United wataingia dimbani
usiku wa leo kuchuana na Olympiakos huku walinzi wake wawili Phil Jones
na Jonny Evans wakishindwa kucheza kutokana na kuwa majeruhi.
Mashetani Wekundu hao kutoka Old
Trafford pia watamkosa kiungo wake mahiri Luis Nani ambae nae ni
majeruhi wakati Rafael na Danny Welbeck wote wakitokea majeruhi
wamejiunga na kikosi cha timu hiyo tayari kupambana na mabingwa hao wa
Ugiriki. Safu ya ushambuliaji ya Man United inatarajiwa kuongozwa na
Wayne Rooney na Robin van Persie huku kiungo Juan Mata aliyesajiliwa
hivi karibuni akishindwa kucheza kutokana na kuzuiwa na kanuni za UEFA
kwa kuwa tayari alishiriki michuano ya msimu huu akiwa na timu yake ya
zamani, Chelsea.
Olympiakos nao watamkosa mfumania
nyavu wao Javier Saviola aliye majeruhi. Hivyo safu ya ushambuliaji wa
timu hiyo itaongozwa na Mnaijeriaa, Michael Olaitan (21).
Japokuwa hali bado ndivyo sivyo kwa
timu ya Olympiakos kwani Nelson Valdez aliyesajiliwa wakati wa dirisha
dogo Januari haileweki kama atakuwa tayari kucheza au la, kocha wa timu
hiyo Michael amesema mchezaji huyo yupo lakini hakuelezea iwapo
atampanga ama la alipoulizwa kuhusu uimara wa mchezaji huyo anayetokea
Paraguay.
Olympiakos, mabingwa wa soka nchini
Ugiriki watakutana na mabingwa kutoka Uingereza, Manchester United
katika uwanja wa Karaiskakis jijini Athens, leo usiku majira ya saa 4.45
kwa saa za Afrika Mashariki.
Michezo itakayochezwa leo usiku katika klabu bingwa ulaya
0 comments:
Post a Comment