Tuesday, 25 February 2014

UCL: MAN UNITED YAPIGWA 2-0! NA OLYMPIACOS YAFUATA NYAYO ZA MAN CITY, ARSENAL,

>>OLYMPIACOS 2 MAN UNITED 0!!
MATOKEO:
Jumanne Februari 25
Zenit St. Petersburg 2 BV Borussia Dortmund 4
Olympiacos CFP 0 Manchester United 2

OLYMPIACOS 2 MANCHESTER UNITED 0
man u fc5adWAKICHEZA huko Karaiskakis Stadium, Jijini Athens, Ugiriki na Olympiakos kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Manchester United walinyukwa Bao 2-0.
Bao za Olympiacos zilifungwa na Alejandro Dominguez katika Dakika ya 38 na Joel Campbell, ambae ni Mchezaji wa Arsenal alieko Olympiacos kwa Mkopo, aliefunga kwa Shuti safi katika Dakika 55.
Robin van Persie alipata nafasi safi kuipatia Bao Timu yake lakini shuti lake la Mguu wake ‘dhaifu’ wa Kulia lilipaa juu.
Man United ni Timu ya 3 ya England, kufuatia Man City na Arsenal, kuchapwa 2-0 kwenye Raundi hii lakini tofauti yao ni kuwa wao wamefungwa Ugenini na watarudiana Nyumbani hapo Machi 19, Man City na Arsenal zitasaka ushindi wa Ugenini kwenye Mechi za Marudiano.
VIKOSI:
OLYMPIACOS: Roberto; Salino, Manolas, Marcano, Holebas; N'Dinga, Maniatis, Dominguez, Fuster, Campbell; Olaitan.
Akiba: Megyeri, Paulo Machado, Samaris, Haedo Valdez, David Fuster, Papadopoulos, Bong Songo.
MAN UNITED: De Gea; Smalling, Ferdinand, Vidic, Evra; Valencia, Carrick, Cleverley, Young; Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Büttner, Fellaini, Giggs, Kagawa, Hernandez, Welbeck.
REFA: Gianluca Rocchi [Italy]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA:
Jumatano Februari 26
[Saa za Bongo]
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC [2-0]
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan [1-0]
Jumatano Machi 12
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City [2-0]
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen [4-0]
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg [4-2]
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]

0 comments: