Msemaji wa kundi la kigaidi la
al-Shabab la nchini Somalia amesema kuwa, wapiganaji wa kundi lake
wanapanga mikakati ya kudhibiti tena maeneo yote ya Somalia ukiwemo mji
mkuu, Mogadishu.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu
na kanali ya Aljazeera ya Qatar, Ali Dheere amesema kujiondoa wapiganaji
wa al-Ahabab katika miji kadhaa ya Somalia hakupaswi kuonekana kama
pigo bali ni mbinu ya wapiganaji hao ya kujipanga upya. Amesema kundi
lake ambalo limetangaza mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda,
halitasalimu amri.
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia
alisema siku chache zilizopita kwamba kundi hilo litaangamizwa kufikia
mwisho wa mwaka huu.
Magaidi wa al-Shabab wiki iliyopita
walishambulia Ikulu ya Rais mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu
14. Wamesema mashambulizi hayo yalikuwa onyo kwa serikali kwamba kundi
hilo bado lina nguvu ya kushambulia sehemu yoyote ndani na nje ya
Somalia.
Chanzo, kiswahili.irib.ir/habari.
0 comments:
Post a Comment