Friday, 28 February 2014

LIGI KUU ENGLAND: CHELSEA KUBAKI KILELENI AU ARSENAL KUIPIKU?

>>WENGER ASISITIZA LIGI KUU ENGLAND NDIO BORA!
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 1
1800 Everton v West Ham
1800 Fulham v Chelsea
1800 Hull v Newcastle
1800 Stoke v Arsenal
2030 Southampton v Liverpool

WENGER_BAADA_KUFUNGWAWAKATI Manchester City hawana Mechi ya Ligi Kuu England Wikiendi hii kwa vile Jumapili wako Uwanjani Wembley kucheza Fainali ya CAPITAL ONE CUP na Sunderland, Chelsea na Arsenal zina nafasi ya kujitanua kileleni kwa kuongeza pengo lao na City kuwa kubwa huku wao wenyewe wakigombea nani atakuwa Nambari Wani.
Jumamosi, Vinara Chelsea, ambao wako Pointi 1 mbele ya Arsenal, watakuwa Ugenini kucheza na Fulham na Arsenal pia wapo Ugenini kuivaa Stoke City.
Liverpool, ambao wako Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Man City, wana nafasi nzuri ya kuipita City ikiwa nao pia watashinda Mechi yao ya Ugenini dhidi ya Southampton.
Everton, ambao wako Nafasi ya 7, watakuwa Nyumbani Goodison Park kucheza West Ham na wakitoka Sare au kushinda wataishusha Man United ambao hawana Mechi Wikiendi hii.
Mabingwa Watetezi Man United Mechi yao inayofuata ya Ligi ni Wikiendi ijayo hapo Machi 8 watakapokuwa Ugenini kucheza na West Bromwish Albion.
WAKATI HUO HUO, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameitetea Ligi Kuu England licha ya Vilabu vyake vinne kuanza vibaya kwenye Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi hizo, Arsenal na Man City zilichapwa 2-0 Nyumbani kwao walipocheza na Bayern Munich na Barcelona na Man United kufungwa 2-0 Ugenini na Olympiacos wakati Chelsea ilipata Sare ya 1-1 huko Uturuki dhidi ya Galatasaray.
Hata hivyo, Wenger amedai Ligi Kuu England ipo kiwango cha juu na ametamka: “Ukweli Ligi hii ni ngumu Duniani kwani kiwango ni kizuri kuanzia Timu ya Kwanza hadi ya Ishirini. Ni Ligi pekee Ulaya ambayo ina hilo. Lazima ujue huko Ulaya Timu zote 4 za England zilifuzu toka Makundi yao. Baada ya Gemu moja huwezi ukaamua ubovu wao! Man City walicheza Mtu 10, Arsenal walicheza Mtu 10. Man City walicheza na Barcelona na Arsenal walicheza na Bayern Munich ambao ndio Mabingwa wa Dunia. Kucheza Mtu 10 ni ngumu! Baada ya hapo Timu nyingine mbili, Man United na Chelsea, bado wako kwenye nafasi kugeuza matokeo, wako Nyumbani!”
Wenger alimaliza: “Ngoja tusubiri matokeo ya Mechi za pili kisha tuanze kusema mwelekeo wa Ligi hii, udhaifu au nguvu yake!”
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 2
1930 Aston Villa v Norwich
1930 Swansea v Crystal Palace
1930 Tottenham v Cardiff
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
27
28
60
2
Arsenal
27
25
59
3
Man City
26
42
57
4
Liverpool
27
35
56
5
Tottenham
27
3
50
6
Man United
27
12
45
7
Everton
26
10
45
8
Newcastle
27
-5
40
9
Southampton
27
6
39
10
West Ham
27
-3
31
11
Hull
27
-2
30
12
Swansea
27
-4
28
13
Aston Villa
27
-10
28
14
Norwich
27
-19
28
15
Stoke
27
-15
27
16
Crystal Palace
26
-18
26
17
West Brom
27
-8
25
18
Sunderland
26
-16
24
19
Cardiff
27
-29
22
20
Fulham
27
-32
21
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 8
1545 West Brom v Man United
1800 Cardiff v Fulham
1800 Crystal Palace v Southampton
1800 Norwich v Stoke
1800 West Ham v Hull
2030 Chelsea v Tottenham

0 comments: