Tip
Top Connection ni moja kati ya makundi yaliyopitia misuko suko ya
wasanii wake kutoka wengi tena kwa kipindi kimoja,kama utavuta
kumbukumbu vizuri mwishoni mwa mwaka 2009 haukuwa mwaka mzuri kwao
maana ilipoteza zaidi ya nusu ya wasanii wake.
Wasanii waliotoka Tip Top kipindi kimoja ni pamoja na Keisha,Z
anto,Spack,Pingu,Mb Dogg na baadhi yao ambao bado walikua
hawajatoka,millardayo.com imeongea na Babu Tale ambaye ni meneja wa
kundi la Tip Top Connection na kwa sasa ndiye meneja wa Diamond
Platnumz.
Swali la MTANDAO HUU Ulikua inahitaji kujua idadi ya wasanii walio tayari kurudi Tip Top
mara baada ya kusikia taarifa za kuwepo kwa taarifa za wasanii hao
kurudi Tip Top,Babu Tale ameanza kwa kusema>>‘Kwa sasa mimi ni
Mfanyabiashara tofauti na zamani nilipokuwa naishi na wasanii tulikuwa
tunaishi kama kaka kwamba matatizo yapo kila mmoja ana matatizo yake
mimi nina matatazo na wasanii nao wana matatzio hizo ni sshemu za
maisha’
‘Hakuna msanii amenipigia akasema anataka kurudi tip top wasanii
wengi wanaokuja kwangu wanasema wanataka tufanye biashara na mimi ni
mfanyabiashara kama wao,tunabaki kwenye biashara kwa sababu kama naweza
kumsimamia msani ambaye sijatoka nae toka mwanzo kwanini yule niliekuwa
nae mwanzo nishindwe kumsimamia na akaleta heshima nchini akapata mkate
wake wa kila siku na mimi nikapata hela’
‘Mpaka sasa wasanii waliokuwa Tip Top wanaotaka kufanya kazi na mimi
ni Spack,Keisha,Mb Dog lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg kwa
macho mawili,Mb dogg ana kipaji watu wanaujua uwezo wa Mb Dogg,Mb Dogg
sio kama amepotea hapana ila hana uongozi anahitaji promo ya nguvu tu
akipata hiyo anarudi kupiga hela kama zamani’.
0 comments:
Post a Comment