Mchezo
wa kuwania kuingia hatua ya 16 bora wa Mashindano ya Klabu Bingwa
Barani Afrika kati ya wenyeji timu ya Young Africans dhidi ya timu ya
National Al Ahly utafanyika kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam huku tayari tiketi za mchezo huo zikinunuliwa kwa wingi na
wapenzi wa soka kwa ujumla.
Young
Africans ambao ndio wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa nchini
Tanzania kawa sasa watashuka dimbani kesho kwa lengo moja tu la
kuhakikisha historia inaandikwa kwa kuvunja mwiko dhidi ya Waarabu na
kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kikosi
cha Mholanzi Hans Van de Pluijm kimekuwa kikiendelea na mazoezi asubuhi
na jioni katika Uwanja wa Boko Beach kujiandaa na mchezo huku morali ya
wachezaji ikiwa i ya hali ya juu, saikolojia na kimwili wakiwa tayari
kwa mechi.
Kuelekea
mchezo wa kesho mchezaji pekee ambaye atakosekana ni Rajabu Zahir
kutokana na kupata maumivu ya kuchanika nyama za msuli wa paja
National
Al Ahly ambao waliwasili jumatano asubuhi leo jioni majira ya saa 10:00
jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa tayari kwa kuuzoea kwa
mchezo wa kesho kufuatia kufanya mazoezi kwa siku mbili katika shule ya
IST Upanga.
Uongozi
wa Young Africans umejiandaa na kuhakikisha kila kitu kinakwenda salama
kwa upande wa wachezaji, utawala na washabiki watakaojitokeza
kushuhudia mchezo huo ulioteka hisia za wapenzi wengi wa soka barani
Afrika.
Mechi
inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika
Mashariki na milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa mapema ili
kupunguza msongamano wa watu watakaojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Wapenzi,
wanachama na washabiki wa soka kwa ujumla wanaombwa kujitokeza kwa
wingi kesho kuja kuipa sapoti timu ya Young Africans kwani ndio timu
pekee inayowakilisha nchi na kupeperusha bendera ya Taifa katika
mashindano ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment