Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Mh. John Mnyika.
Maoni
yangu kuhusu matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne wa
mwaka 2013 yaliyotangazwa na kuelezwa kuwa ufaulu umeongezeka kwa
asilimia 15.17 yamedhihirisha tahadhari niliyotoa kuhusu mabadiliko ya
viwango vya ufaulu yaliyotangazwa na Serikali tarehe 30 Oktoba 2013.
Serikali
kwa barakoa (veil) ya kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big
Results Now) imeamua kulificha taifa juu ya Matokeo Mabaya ya Sasa (Bad
Results of Now). Hivyo, wachambuzi wa masuala ya elimu wanapaswa
kutoa takwimu za matokeo yangekuwa namna gani iwapo viwango vya awali
vya ufaulu vingetumika ili
nchi ijue hali halisi kwa manufaa ya wananchi.
nchi ijue hali halisi kwa manufaa ya wananchi.
Aidha,
natoa mwito kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuweka wazi kwa umma
ripoti za uchunguzi zilizoundwa kuwezesha wananchi kuihoji Serikali
iwapo kupanda huko kwa ufaulu ni matokeo ya kuboresha mazingira ya
kufundisha na
kujifunza au ni kiini macho cha mabadiliko ya wigo wa alama na madaraja?
kujifunza au ni kiini macho cha mabadiliko ya wigo wa alama na madaraja?
Ukweli
ni kuwa hali ya mazingira ya kujifunza na kujifunzia katika
shule nyingi za msingi na sekondari hasa za umma sio nzuri kutokana na
kutokuwa na vitabu vya kutosha, maabara za kutosha, waalimu wenye sifa
wapo wa kutosha na kuboresha maslahi ya waalimu ambayo yamekuwa
yakilalamikiwa kwa siku nyingi.
Ikumbukwe
kwamba miaka mitatu mfululizo, mfumo wa elimu wa Tanzania, na hususani
kwa upande elimu ya msingi na sekondari umekuwa ukiporomoka kwa kasi ya
ajabu. Kufuatia kuporomoka huko, na hasa kushuka kwa viwango vya
ufaulu, Serikali kwa vipindi totauti (mwaka 2010 na 2012) imeund Tume kuchunguza sababu za kushuka kwa viwango vya ufaulu.
ufaulu, Serikali kwa vipindi totauti (mwaka 2010 na 2012) imeund Tume kuchunguza sababu za kushuka kwa viwango vya ufaulu.
Ingawa
ripoti za tume zilizoundwa kuchunguza sababu za kushuka kwa ufaulu
hazijulikani kwa wananchi ambao ni wadau wakuu wa elimu,
Serikali imeendelea kutoa maagizo na matamko mbalimbali kuhusu viwango
vya ufaulu.
Ikumbukwe
kuwa mwezi Mei, 2013 Serikali ilitangaza kufutwa kwa matokeo ya kidato
cha nne ya mwaka 2012 kutokana na kushuka mno kwa viwango vya
ufaulu ambapo zaidi ya asilimia 65 ya wanafunzi walipata daraja sifuri
na kuamuru
matokeo hayo kupangwa upya.
matokeo hayo kupangwa upya.
Takribani
miezi sita baadaye, yaani 30 Oktoba 2013 Serikali ilitangaza kubadili
viwango vya ufaulu bila kutoa ufafanuzi kuhusu msingi wa mabadiliko hayo
na kuwasilisha bungeni ripoti za kamati/timu zilizochunguza kuporomoka
kwa ufaulu.
Hivyo
hata baada ya kauli ya Serikali kuwa “kundi la watahimiwa walioshindwa
Mtihani na ambalo awali lilikuwa likiandikwa kama ‘failures’ litaendelea
kujulikana kama Daraja Sifuri (Zero) bado Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi inapaswa kutoa ufafanuzi juu ya athari za mabadiliko
hayo kuwezesha Bunge kusimamia Serikali ipasavyo.
Pamoja
na mpango wa Serikali wa kuficha matokeo mabaya ya kidato cha nne
ya mwaka 2013 bado idadi ya waliofeli imeendelea kuwa kubwa kwa
kuwa watahiniwa 151,187 sawa na asilimia 42.91 wamepata sifuri. Kati ya
hao, wavulana ni 78,950 sawa na asilimia 41.54 na wasichana ni 72,237
sawa na asilimia 44.51. Aidha, katika matokeo hayo hali ya watahiniwa
kutokuweza kufanya mtihani kabisa kwa kiwango cha kuacha karatasi tupu,
kuchora vitu vya ajabu au kuandika matusi inadhihirisha udhaifu mkubwa
uliopo katika mfumo wetu wa elimu kwa kuwa wahusika wameweza kupanda
kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne wakiwa hawana uwezo wa kufanya
mitihani.
Hivyo,
Serikali ihojiwe ieleze dhamira ya kweli ya mabadiliko ya viwango vya
ufaulu na kutakiwa kushughulikia vyanzo vya matatizo katika elimu badala
ya kuficha matokeo mabaya na hali halisi za wahitimu.
Serikali
inafanikiwa kuficha udhaifu kwa sababu ripoti kamili za uchunguzi juu
ya ufaulu duni wa wanafunzi hazijawahi kuwekwa hadharani ili kujua kiini
cha tatizo. Mara zote Serikali imekuwa ikifanya maamuzi bila kuzingatia
ripoti za uchunguzi na ndio maana Serikali haikusita kuunda tume ya
kuchunguza sababu za kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne 2012
wakati kulikuwa na tume iliyofanya kazi hiyohiyo mwaka 2010.
Endapo
tutaendelea kufikiri kwamba kulegeza njia za ufaulu ndio
kuboresha elimu, tutajikuta tuna taifa la watu wenye vyeti vizuri vya
elimu lakini wasioweza kufanya kazi inayoshabihiana na alama za ufaulu
katika vyeti vyao.
Wataalamu
wa elimu waitake Serikali kuacha kufanya mambo yanayohitaji utaalamu
kwa ajili ya kujitafutia sifa kisiasa kwa mipango mibovu. Suala la elimu
lisichukuliwe kama ajenda ya siasa chafu kwani kwa kufanya hivyo
tunaiua elimu yetu.
tunaiua elimu yetu.
Ni
vema kabla Serikali haijafanya maamuzi ya jambo linaloathiri maisha
ya watanzania wengi kama hili la mitihani ikaleta kusudio la kufanya
hivyo bungeni ili wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wajadili na
kuishauri Serikali Ipasavyo.
Mwisho
kabisa, napenda wananchi wafahamu kwamba kwa mujibu wa
kitabu kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka cha
“International Qualification”, baada ya Tanzania kutangaza alama mpya za
ufaulu, sasa inakuwa nchi inayoongoza duniani kwa kuwa na alama za
chini za ufaulu. Maana yake ni kwamba, tumeshusha ubora na thamani ya
elimu yetu.
Hivyo
naitaka Serikali kutoa ufafanuzi ni kwanini isifute uamuzi wake
wa kubadili viwango vya ufaulu ambayo tayari umeanza kuficha hali hali
ya matokeo mabaya katika mitihani. Na badala yake itoe kwa umma na
iwasilishe bungeni ripoti za uchunguzi zilizoundwa na kuliwezesha Bunge
kufanya maamuzi ya kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)
22/02/2014
22/02/2014
0 comments:
Post a Comment