Mabaki ya chuo cha serikali ambapo wanafunzi 60 walichomwa moto hadi kufa Februari 25, 2014
Shambulizi hilo la Alhamis karibu na
mpaka wa Cameroon lilifanyika siku moja baada ya mashahidi kuripoti kuwa
takribanu wanafunzi 60 waliuwawa katika chuo cha serikali.
Mashahidi na maafisa wa ndani
kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kundi linalotuhumiwa la
wanamgambo wa Boko Haram limeuwa watu 33 na kushambulia kwa bomu chuo
cha kidini katika jimbo la Adamawa.
Jeshi ambalo mara nyingi haliamini
taarifa za idadi ya vifo kutoka kwa mashahidi limesema washambuliaji
sita waliuwawa katika tukio hilo pamoja na mwanajeshi mmoja na raia
watatu .
Shambulizi hilo la Alhamis karibu na
mpaka wa Cameroon lilifanyika siku moja baada ya mashahidi kuripoti kuwa
karibu wanafunzi 60 waliuwawa katika chuo cha serikali karibu na jimbo
hilo la Adamawa.
Chanzo, voaswahili
0 comments:
Post a Comment