Mhandisi
wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha
taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya
5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu
Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence
Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi
Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia). Viongozi
wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na
Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu
Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia)
wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi. Kaimu
Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (Kulia)
akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia
zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na
wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Kaimu
Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William
(aliyenyanyua mkono) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya tanki la
kuhifadhia maji kwa ajili ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya
kaya 5000 za manispaa ya Iringa. Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wa Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) ambao ni wanufaika wa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa , Bw. Ranier Nyimbo (Mwenye Fulana nyeusi) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwenye uwanja huo. Baadhi
ya wanavijiji wa Nduli na Kigonzile kutoka manispaa ya Iringa wakichota
maji katika bomba pekee linalopatikana katika mpaka wa vijiji hivyo.
Adha hii itaisha mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa
mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ikiwemo
wanavijiji hawa. Mhandisi
wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Watatu Kulia)
akiwaonesha wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango moja ya
mabomba yatakayotumika kusambaza maji.
PICHA NA SAIDI A. MKABAKULI
………………………………………………………………………………………..
Katika
kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016),
Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi
ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa
fedha.
Hayo
yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya
Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na
wafadhili.
Bibi
Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali
inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya
maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa
katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili
kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi
vyanzo vya maji.
Akizungumza
wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa,
Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa
Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na
miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.
Maji
ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa
Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango. Maeneo mengine
ya
vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya
usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na
huduma za jamii.
0 comments:
Post a Comment