Toleo
jipya la Fuso aina ya FJ ikiwa kwenye muundo wa tipper lenye uwezo wa
kubeba tani 25 maalum kwa ajili ya sekta ya ujenzi na uchimbaji wa
madini.
Toleo jipya la Fuso aina ya FI lenye uwezo wa kubeba tani 12.
Aina mbalimbali za Fuso zilizoingia nchini tayari kutoa suluhisho na Changamoto za kimaendeleo hapa nchini.
Sekta
ya usafiri nchini inatarajiwa kuwa na mabadiliko makubwa baada ya
kampuni ya uwakala wa magari ya Diamond Motors Limited (Sehemu ya Hansa
Group) kutambulisha aina mpya ya magari ya Fuso yenye uwezo wa kubeba
mizigo yenye uzito mkubwa na ya kati katika soko la Tanzania.
Katika
miaka ya hivi karibuni sekta za usafiri, madini, kilimo na ujenzi
imechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa Uchumi nchini huku ikishuhudiwa
ushindani mkubwa wa kibiashara kwa makampuni ya magari ya kimataifa
ambapo aina hizi za Fuso zinatarajiwa kuongeza kasi ya ushindani Kwani
gari zote zimetengenezwa kuongeza faida kwa mteja.
Akitoa
Maelezo ya kina ya Fuso mpya, Meneja Mkuu wa Diamond Motors Limited
nchini Tanzania ambao ndio wasambazaji wakuu wa magari ya Fuso, Bw.
Vikram Verma alisema kuwa soko la Tanzania litarajie kupata faida kubwa
kutokana na ujio mpya wa Fuso FA, FI, na FJ. Ikiwa na injini iliyoundwa
kuhimili uzito na mazingira magumu, matoleo haya yanampa mtumiaji
thamani ya juu.
Toleo
la FA ina uwezo wa chini, wenye kubeba mzigo wa tani 9, toleo FI yenye
uwezo wa kubeba tani 12 na FJ inao uwezo wa kubeba tani 25 ambapo FA ina
muundo mmoja, wakati toleo la FJ na FI ina miundo miwili inayokuruhusu
kufanya kazi katika sekta tofauti
“Tuna
nia ya kuunga mkono maendeleo ya uchumi wa Tanzania na juhudi za
wawekezaji, Fuso yetu mpya imetengenezwa kuleta mapinduzi katika sekta
ya usafirishaji Tanzania. Aina mpya wa Fuso sio tu yenye ubora wa
kuaminika bali yenye uwezo wa kipekee wa kubeba mzigo, tofauti na malori
mengine yenye uwezo kama wa Fuso, utatumia kiasi kidogo cha mafuta na
gharama ndogo za matengenezo. Hayo ndio yanayofanya Fuso kua tofauti na
njia nyingine za usafirishaji katika biashara zilizopo Tanzania”,
alisema Vikram Verma katika Mahojiano.
Maendeleo
ya uchumi wa Tanzania unasisitiza uhitaji wa njia bora za usafirishaji
ikiwa uchumi unaendelea kukua kila siku. Kumekua na Juhudi za serikali
kutengeneza miundombinu na huduma zinazosaidia kukua kwa biashara za nje
na ndani na kuimarisha mahusiano na uwekezaji kutoka nje ya Tanzania.
Fuso
zote za uwezo wa kati na mkubwa, zina ubora wa kimataifa, zilizopitia
majaribio ikiwemo kuendeshwa zaidi ya kilomita milioni 9. Lori hili lina
injini na nguvu ambayo imetengenezwa kuhimili mazingira na imeundwa kwa
teknolojia za kisasa kutoka Japani na Ujerumani ikiwemo teknolojia ya
Common Rail.
Fuso
imekua rafiki wa mazingira kwa kukupatia lori lenye utoaji mdogo wa
gesi ya kaboni. Ikikupatia muda mrefu wa matengenezo, spea zinazodumu
muda mrefu na gharama ndogo za matengenezo ununuapo Fuso yenye uwezo wa
kati au mkubwa unakua na uhakika wa kupata faida.
0 comments:
Post a Comment